HABARI KUU
Maafisa nchini Nigeria wamethibitisha kuokolewa kwa watu 137 waliotekwa na watu wenye silaha huko Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo wiki mbili zilizopita.
Taarifa zimeeleza kuwa operesheni ya uokoaji ilifanyika alfajiri ya leo ikiwa ni siku chache kabla ya tarehe ya mwisho ya malipo yaliyoombwa na watekaji hao.
Gavana wa Jimbo la Kaduna Uba Sani amesema wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa shule wameokolewa kutokana na ujasiri wa maafisa wa usalama.
Wiki iliyopita majambazi hao walidai kiasi cha pauni 486,000 ili kuwaachia watu hao, hata hivyo Rais Bola Tinubu aliahidi kuwaokoa bila ya kulipa hata senti moja.
Idadi ya wanafunzi na wafanyakazi wa shule waliotekwa katika wiki za hivi karibuni ni 287 hivyo takribani nusu yao bado wanashikiliwa mateka.
Majambazi hao wamekuwa wakiwateka nyara maelfu ya watu katika miaka ya hivi karibuni nchini humo na kuwaachia huru mara baada ya kulipwa.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.