KATIBU MKUU WA CCM BADO ASHIKILIA MSIMAMO WA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR

0:00

HABARI KUU

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amesema uamuzi wa kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar ulizingatia kutanguliza mbele usalama wa maisha ya watu, maslahi, utulivu na mstakabali mwema wa Zanzibar, Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujumla, kuliko vyama vya siasa.

Balozi Dk. Nchimbi amesema uwepo wa Serikali hiyo Zanzibar umeondoa hali ya siasa za chuki na uhasama mkubwa uliokuwepo kabla ya kufikiwa kwa uamuzi wa kuundwa kwake, huku akisisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kutimiza wajibu wake wa kutoa uongozi kwa nchi ili kudumisha umoja na utulivu uliokusudiwa kwa maslahi ya Wazanzibar na Watanzania wote.

Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akizungumza na Wazee wa Zanzibar, Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, leo Jumapili, Machi 24, 2024, ikiwa ni siku ya pili akiwa kwenye ziara ya kikazi.



“Binafsi nikimsikia mtu anazungumzia kutaka kujitoa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa, simwelewi huyo mtu hata kidogo. Kwa sababu Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilikuwa kwa ajili ya usalama wa maisha ya watu, usalama wa Wazanzibar, usalama wa Watanzania. Maisha ya watu ni muhimu sana kuliko kitu chochote kwanza. Tuliweka mbele maslahi ya nchi, utulivu na umoja wetu, si vyama vya siasa.

“Mnakumbuka wakati fulani nikiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kila siku nenda rudi kwa helkopita kuja Zanzibar. Tulikuwa tunahangaika kuondosha uhasama na chuki. Najua kuna wakati wenzetu wanapata gadhabu na kuzungumza kwa jazba. Sisi wanaCCM tusiende huko hata kidogo. Sisi ndiyo Chama tawala. Sisi ni walezi. Mlezi hasusi. Tusiache wajibu wetu wa kulea hata kidogo. Mtoto ndiye anasusa. Na katika hili naombeni sana wazee wote wa Zanzibar na Tanzania, mniunge mkono,” amesema Balozi Dk. Nchimbi.

See also  IRAN yaweka masharti mapya kwa mavazi ya Wanawake



Aidha, Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi pia amesisitiza msimamo wa CCM kuendeleza kutimiza wajibu wa kipekee wa kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na misingi yake.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Environment CS Nominee Declares Corruption Greater Threat...
Aden Duale, the nominated Environment Cabinet Secretary of Kenya, has...
Read more
President Ruto Reshuffles Kenya Defence Forces Leadership...
President William Ruto has announced a significant reshuffle within the...
Read more
WATU 9 WAFARIKI BAADA YA GARI LAO...
HABARI KUU Watu tisa wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa...
Read more
RWANDA KUONGOZA UKUAJI UCHUMI KWA AFRIKA MASHARIKI...
MAKALA Ripoti ya Ukuaji wa Uchumi iliyotolewa na Benki ya Maendeleo...
Read more
Sauber sign Brazilian Bortoleto to complete F1...
Formula One will have a full-time Brazilian driver for the...
Read more

Leave a Reply