WALIOFANYA SHAMBULIZI NCHINI URUSI WAKAMATWA WANNE

0:00

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

HABARI KUU

Serikali ya Urusi, imewafungulia mashtaka watu wanne wanaodaiwa kufanya shambulizi katika ukumbi wa Crocus City Hall jijini Moscow usiku wa kuamkia Machi 23, 2024 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 130 karibu na jiji la Moscow.

Watu hao wamefunguliwa mashtaka ya ugaidi katika Mahakama ya Wilaya ya Basmanny mjini Moscow ambapo huenda wakakabiliwa na hukumu ya maisha jela, lakini wataendelea kubaki kizuizini hadi Mei 22, 2024 kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo inayowakabili.

Taarifa ya Mahakama imewataja washtakiwa hao kuwa ni Dalerzdzhon Mirzoyev (32), Saidakrami Rachabalizoda (30), Shamsidin Fariduni (25) na Mukhammadsobir Faizov (19) na wawili kati yao walikiri kuhusika na shambulizi hilo.

Hata hivyo, watu hao walionesha dalili za kuwa hoi kwa kipigo, huku kukiwa na shaka kuhusu uhuru waliokuwa nao wakati wakijibu maswali waliyokuwa wakihojiwa.

Related Posts 📫

Opposition in Disarray as Four Members Nominated...
The opposition appears to be in a state of limbo...
Read more
Pep Guardiola has made it clear he...
The striker has starred for City since arriving in the...
Read more
MESSI KUWEKA REKODI HII MPYA ...
MICHEZO Nyota wa soka Lionel Andres Messi huenda akaongeza rekodi...
Read more
Verstappen more worried about his pace than...
MEXICO CITY, - Max Verstappen sounded more concerned about his...
Read more
Convener of the Yoruba Nation movement, Chief...
In a statement yesterday, Igboho defended President Bola Ahmed Tinubu’s...
Read more
See also  MWANASIASA WA UPINZANI AKUTWA AMEFARIKI

Leave a Reply