MACKY SALL AMPONGEZA BASSIROU DIOMAYE FAYE KUSHINDA URAIS

0:00

HABARI KUU

Rais wa Senegal anayemaliza muda wake, Macky Sall amempongeza mgombea wa upinzani, Bassirou Diomaye Faye kwa ushindi alioupata huku mshindani wake wa karibu, Amadou Ba akikubali kushindwa katika uchaguzi huo.



Baada ya mgombea huyo wa chama tawala, Amadou Ba kutambua ushindi wa Faye katika duru ya kwanza na kutoa pongezi zake, Sall, ambaye alishinda chaguzi za mwaka 2012 na 2019, amesema “napongeza maandalizi mazuri ya uchaguzi na nampongeza mshindi, Bassirou Diomaye Faye ambaye mwenendo wa kura unaonyesha kwamba ameshinda.”

Mgombea huyo wa upinzani aliyeshinda hajawahi kushika nafasi ya kuchaguliwa ya kitaifa na bado hajazungumza hadharani tangu uchaguzi wa Jumapili Machi 24, 2024, uliofuatia miaka mitatu ya machafuko na mgogoro wa kisiasa.

Mpinzani wake mkuu kutoka muungano wa chama tawala, Amadou Ba ametambua ushindi wa Faye katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo na akatoa pongezi zake, ilisema taarifa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

DRC NAMES JUDITH TULUKA SUMINWA AS A...
TOP NEWS President Félix Tshisekedi has just appointed Judith Tuluka Suminwa...
Read more
Orodha ya washindani wa Paul Kagame uchaguzi...
SIASA Tume Huru ya uchaguzi nchini Rwanda imewaidhinisha watu watatu katika...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 18,2023...
Magazeti Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye kurasa za leo...
Read more
LOKASSA YA MBONGO AJAZIKWA MIEZI 6 BAADA...
Nyota wetu Aliyekuwa gwiji mcharaza gitaa maarufu wa Jamhuri ya kidemokrasia...
Read more
Sababu zinazosababisha "Allergy " /mzio
Mzio hutokea pale mwili unapopambana na kitu kisicho na madhara...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  KATUMBI APINGA USHINDI WA TSHISEKEDI

Leave a Reply