HISTORIA YA BASSIROU DIOMAYE FAYE RAIS MTEULE WA SENEGALimg

0:00

HABARI KUU

Mgombea Urais kutoka kambi ya upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ndiye Rais mpya wa Senegal baada ya kushinda Uchaguzi wa Rais nchini humo ikiwa ni wiki moja baada ya kutoka Gerezani.

Faye amechaguliwa kuwa Rais mteule wa taifa hilo akiwa na umri wa miaka 44 ambaye ataapishwa kuwa Rais wa Taifa hilo.

Rais huyo ameweka historia ya kuwa Rais mwenye umri mdogo zaidi barani Afrika na katika uchaguzi huo, maelfu ya Wasenegali walijitokeza katika maeneo mbalimbali wakisubiri kwa utulivu kupiga kura zao.

Abdoulaye Sylla, Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi amesema idadi kubwa ya watu walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo.

Mgombea wa ushirika wa utawala nchini Senegal ambaye alikuwa mgombea mwenzake kwenye nafasi hiyo, Amadou Ba amempongeza mpinzani wake kutoka kambi ya upinzani, Faye kwa kushinda uchaguzi wa Rais.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SABABU 10 ZA MIMBA KUHARIBIKA
AFYA " HIZI HAPA SABABU KUMI MUHIMU ZA MIMBA KUHARIBIKA...
Read more
MBUNGE DKT. MLOZI KUZIKWA MANYARA, AACHA PACHA...
Mazishi ya Aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika...
Read more
JEZI YA GREENWOOD YAVUNJA REKODI YA MAUZO...
Nyota wetu Imeripotiwa kuwa jezi ya mchezaji mpya wa klabu ya...
Read more
RAIS SAMIA ANAJENGA ALIPOBOMOA MAGUFULI
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Kenya Railways Unveils Luxurious SGR Executive Coaches...
The Kenya Railways has introduced new SGR (Standard Gauge Railway)...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Kwanini Obama na Michelle Wanamuunga Mkono Kamala?

Leave a Reply