Polisi wa Argentina wanachunguza vitisho vya kifo vilivyotolewa kwa familia ya mshambuliaji Angel Di Maria nyumbani kwao Roasario.

0:00

Wafanyakazi kwenye nyumba ya staa huyo mshindi wa Kombe la Dunia na Argentina mwaka 2022, walisema walikutana na ujumbe uliokuwa na vitisho vya vifo kama ataendelea kucheza kwenye moja ya klabu katika mji wa Rosario.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 36 anayecheza Benfica ya Ureno hivi karibuni alisema anaweza kurejea kucheza kwenye klabu yake ya utoto ya Rosario Central. Kwa sasa yuko Marekani na timu ya taifa ya Argentina.

“Vitisho kama hivi vinasababisha usumbufu mwingi kwenye jamii na hilo ndio lengo lake, kufanya wananchi wawe na hofu, kuwatisha watu muhimu kwenye jamii,” alisema Esteban Santantino, anayefanya kazi kwenye vyombo vya usalama katika mji wa Rosario.

Vyombo vya habari vinasema malengo ya vitisho hivyo bado hayako wazi, ingawa Polisi walishindwa kukataa taarifa zozote za uchunguzi.

Di Maria alianza kwenye mchezo wa jana wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Costa Rica kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo, Lionel Scaloni.

“Di Maria anafahamu tuko nyuma yake kwa chochote atakachohitaji. Kitu muhimu ni kwamba alicheza, hicho kitamfanya apate faraja kidogo.

Rosario imekumbwa na matukio ya vurugu nyingi miongoni mwa magenge yanayohusika na uuzaji wa dawa za kulevya. Mauaji ya watu kwenye mji huo ni watu 22 kwa 100,000.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KWANINI MAHUJAJI WANAKUFA KWENYE MIJI YA MAKKAH...
HABARI KUU Mamia ya mahujaji wamefariki dunia na maelfu wanatibiwa...
Read more
HUNTER BIDEN AKUTWA NA HATIA YA...
Hunter Biden (54), ambaye ni mtoto wa Rais wa Marekani...
Read more
Yanga Yanasa Sahihi ya Mtambo wa Mabao...
Rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi ameiomba klabu ya Yanga...
Read more
Suna East Residents Demand Urgent Road Repairs
The residents of Suna East Constituency in Migori County have...
Read more
RAIS WA ANGOLA AZUA SINTOFAHAMU KENYA ...
HABARI KUU
See also  Sababu Zilizosababisha Vijana Uganda Kuandamana
Kumekuwa na sintofahamu nchini Kenya baada ya...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply