UMMY MWALIMU ATAJA MAFANIKIO YA WIZARA YA AFYA KWENYE UTAWALA WA RAIS SAMIA

0:00

HABARI KUU

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema sekta ya afya imekua kwa kiwango kikubwa kwenye miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan kiasi cha kuvutia watu kutoka nchi jirani kuja kutibiwa Tanzania ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Waziri Ummy amesema Sekta ya Afya kwa sasa imejikita zaidi kwenye tiba za kisasa na kwamba kwa upande wa vipimo ambapo mashine za CT-Scan zimeongezwa kutoka 13, kisha 32 na sasa ziko 45 kwa nchi nzima.

Kwa upande wa Ultra sound amesema kwa sasa zinapatikana mpaka kwenye zahanati ambapo kabla ya Rais Samia kuingia madarakani kulikua na mashine za ultra sound 476 ila sasa zipo 665 na kwamba zinasaidia sana matibabu hasa kwa mama wajawazito.

Upande wa mashine za moyo amesema tumetoka kwenye mashine moja mpaka nne, kiasi cha kuvutia nchi nyingi kuja kupata huduma za afya nchini ikiwemo Malawi, Uganda, Kenya, Comoro, Burundi na nyingine nyingi.

Waziri Ummy amesema hayo jijini DSM mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye kilele cha Wiki ya Kurasa 365 za Mama Vol. 3 iliyoandaliwa na Clouds Media Group. Ametumia wasaa huo kuwataka Watanzania kufanya mazoezi na kupunguza matumizi ya vyakula vya mafuta, sukari, chumvi na wanga ili kutunza afya zao.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kwanini Msanii SNURA wa Majanga Amepiga Marufuku...
Mwanamuziki Snura Mushi ametangaza kuacha muziki huku akikataza nyimbo zake...
Read more
Mfahamu Mrithi wa Ugombea Urais wa Marekani...
Rais wa Marekani Joe Biden amesema atasimama na Makamu...
Read more
Kizz Daniel officially announces the end of...
Nigerian singer Kizz Daniel, whose real name is Daniel Anidugbe...
Read more
Content creator Kuye Adegoke enjoyed some quality...
Content creator, Egungun, expressed excitement after spending time with renowned...
Read more
Radamel Falcao mbioni kuiacha Rayo Vallecano
MICHEZO
See also  15 THINGS YOU MUST GIVE YOUR SPOUSE
Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa klabu za Chelsea na Manchester...
Read more

Leave a Reply