ORODHA YA WACHEZAJI WA YANGA AMBAO WAKO HATARINI KUIKOSA MAMELODI SUNDOWNS

0:00

MICHEZO

Pacome, Aucho, Yao hatarini kuwakosa Masandawana



“Natarajia kuwakosa baadhi ya wachezaji wangu nyota. Siwezi kuhatarisha afya za wachezaji ambao bado hawana utimamu wa kimwili. Lakini kuna uwezekano mkubwa wa kukosa wachezaji watatu mpaka wanne,” amesema Kocha wa Yanga SC, Miguel Gamondi kuelekea mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns Machi 30 mwaka huu.



Amesema wachezaji ambao wako hatarini kukosa mchezo huo ni Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Yao Kouassi na Pacôme Zouzoua kutokana na majeraha.

Aidha, amesema anatumaini kuwa Djigui Diarra na Aziz Ki ambao wamerejea leo watakuwa wapo salama na kwamba uamuzi wa mwisho kuhusu hatma ya wachezaji hao utajulikana leo katika mazoezi ya mwisho.



“Licha ya kukosa nyota wangu kwenye maandalizi, nina imani na wachezaji wengine ambao wapo kambini. Jambo muhimu ni kujitoa zaidi, kuliko Mamelodi. Sisemi kuwa hatuwafikii uwezo Mamelodi, ila naamini wana wachezaji wenye uzoefu mkubwa hivyo ni lazima vijana wangu wajitoe zaidi,”

ameeleza Gamondi.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

President Ruto Pledges Support for Kenyans Seeking...
President William Ruto has expressed the government's commitment to supporting...
Read more
AC MILAN YAMKANA TONALI
MICHEZO Klabu ya Ac Milan imetangaza haikuwa inafahamu chochote kuhusu...
Read more
WAASI WA CONGO WAWEKEWA VIKWAZO NA UMOJA...
HABARI KUU Umoja wa Mataifa umeweka vikwazo vya usafiri, silaha...
Read more
MARAIS 10 WA AFRIKA WALIOFIA MADARAKANI ...
MAKALA Baada ya siku ya leo nchi ya Namibia 🇳🇦...
Read more
NEYMAR NA KOCHA WAKE HAWAIVI CHUNGU KIMOJA...
Michezo Nyota wa timu ya Al-Hilal ya nchini Saudia Arabia,...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  BONDIA MTANZANIA DULLA MBABE APIGWA KWA KNOCK OUT

Leave a Reply