SABABU ZIWA TANGANYIKA KUFUNGWA MIEZI MITATU

0:00

HABARI KUU

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza kutekeleza mpango wa kulipumzisha Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma kuanzia Mei 15 hadi Agosti 15, 2024 ambapo shughuli za uvuvi zitazuiwa katika kipindi hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Salum Kalli, amewaambia wadau, viongozi na wavuvi wanaotumia ziwa hilo kuwa zoezi hilo ni sehemu ya kukuza sekta ya uvuvi nchini, kwa kuwa hatua hiyo itasaidia ongezeko la samaki na soko katika siku za usoni kutokana na uwepo wa samaki wa kutosha.

Kalli, amesisitiza juu ya umuhimu wa zoezi hilo katika Ziwa Tanganyika akisema ni kitovu cha mazao ya samaki kutokana na mazalia kuwa mengi na yenye kukidhi mahitaji ya watumiaji.

Ofisa Uvuvi Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ambakisye Simtoe amewataka wadau wa uvuvi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha juu ya kupumzishwa kwa Ziwa Tanganyika ili kuchochea ongezeko la samaki katika ziwa hilo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MWANAUME AWAPA WANAWAKE WATANO UJAUZITO KWA MARA...
NYOTA WETU. Lizzyash Ashliegh ,ambaye ni chanzo cha kusambaa kwa...
Read more
TIWA SAVAGE'S SON ,JAMIL CONCERNED ABOUT THOSE...
OUR STAR 🌟 Jamil Balogun, the only son of the...
Read more
Sababu ya kifo cha Director Khalfani Khalmandro
NYOTA WETU Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamnu Muhimbili...
Read more
ROSE WARDINI AJIONDOA KUGOMBEA URAIS WA SENEGAL...
HABARI KUU Senegal bado ipo katika hali ya sintofahamu baada...
Read more
Latham hails Ravindra impact as New Zealand...
BENGALURU, - New Zealand's first victory in India for 36...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Federal Government has prohibited underage girls from staying in hotels.

Leave a Reply