HABARI KUU
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limetoa taarifa ya hitilafu ya kivuko cha abiria MV Malagarasi kinachofanya shughuli ya kuvusha abiria na mizigo mto Malagarasi eneo la llagala, Wilayani Uvinza ambapo muda wa saa 10:30 Asubuhi kikiwa kinavusha abiria injini za kivuko hicho zilizima ghafla kupelekea kusombwa na maji na kuzua taharuki kwa abiria.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, SACP Filemon K. Makungu imebainisha kuwa jitihada za kuokoa abiria na mizigo zimefanyika kwa ushirikiano baina ya vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi, hakuna madhara yeyote yaliyojitokeza kwa abiria na mizigo.
“Adha, mafundi wamefanikiwa kufanya matengenezo ya injini hizo kisha kivuko hicho kurejea eneo la maegesho.”
“Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linatoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuwa watulivu na kuondoa hofu badala yake waendelea kutekeleza majukumu yao ya kujiletea maendeleo.”
imesema taarifa hiyo.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.