PRINCE DUBE AWASHITAKI AZAM FC SHIRIKISHO LA MPIRA NCHINI TFF

0:00

MICHEZO

Taarifa za uhakika ambazo zimetufikia zinasema kuwa mshambuliaji wa Azam FC aliyeaga klabuni hapo Prince Mpumelelo Dube ameamua kuwashitaki Azam FC kwa shirikisho la mpira nchini TFF.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mshambuliaji huyo ameukana mkataba ambao Azam FC wanasema aliusaini na unaisha mwezi Juni 2026.

Mshambuliaji huyo ametinga TFF na mkataba ambao anasema ni halali ambao unafikia ukomo wake mwisho mwa msimu huu yaani Juni 2024 na kuukana ule ambao Azam wanasema alisaini wa muda mrefu.

Mshambuliaji huyo amepeleka mkataba alionao na ambao anautambua yeye, nyaraka mbalimbali pamoja na vielelezo vingine kuthibishisha kuwa mkataba wake halali anaoutambua ni alionao unaotamatika mwishoni mwa msimu huu.

Hivi karibuni mchezaji huyo aliwaaga Azam kupitia akaunti yake ya Instagram huku akiwashukuru watu mbalimbali katika klabu hiyo kama viongozi wa timu, idara mbalimbali pamoja na mashabiki wa klabu hiyo.

Klabu ya Azam ilijibu mapigo Kwa kusema mshambuliaji huyo bado ni mchezaji wao kwani anao mkataba mrefu na wauza ice cream hao mpaka 2026.

Klabu hiyo imeenda mbali na kumwambia mchezaji huyo kuwa kama anataka kuondoka afuate utaratibu wa kuvunja mkataba na sio kuaga akiwa bado ni mali yao.

Kwa kujibu wa klabu hiyo ni kwamba thamani ya kuvunja mkataba wa mchezaji huyo ni 700m hivyo afike mezani na atimize matakwa ya kifungu hicho ili wamuachie huru.

Taarifa ambazo tunazo ni kuwa Azam FC imekuwa ikimuandikia barua mshambuliaji huyo kila baada ya siku tatu ikimhitaji aripoti kazini kuendelea na majukumu yake.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MATESO ANAYOPITIA RAIS ALIYEPINDULIWA NA JESHI...
HABARI KUU
See also  Chelsea yamfukuza Mauricio Pochettino
Rais wa Gabon aliyeondolewa madarakani, Ali Bongo pamoja...
Read more
KEVIN DE BRUYNE AACHWA UBELGIJI
MICHEZO Kevin De Bruyne ameachwa nje ya kikosi cha Ubelgiji...
Read more
Emilio Nsue López atangaza kurejea kwenye soka
MICHEZO Kinara wa ufungaji kwenye Fainali za Mataifa ya Bara...
Read more
Lagos State Governor Babajide Sanwo-Olu has issued...
The governor’s reaction comes five days after the campaign was...
Read more
Mwenyekiti UVCCM Kagera ashinikizwa kujiuzulu kisa hiki
HABARI KUU VIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply