BASSIROU DIOMAYE FAYE AAPISHWA RASMI KUWA RAIS WA SENEGAL

0:00

NYOTA WETU

Mwanasiasa wa mrengo wa kushoto, Bassirou Diomaye Faye, ameapishwa hii leo kuwa rais wa tano wa Senegal na kuahidi mabadiliko ya kimfumo, uhuru na utulivu baada ya miaka kadhaa ya machafuko.

Sherehe za kuapishwa kwake zimefanyika katika mji mpya wa Diamniadio, karibu na mji mkuu Dakar.

Faye mwenye umri wa miaka 44, ambaye anakuwa rais kijana zaidi kuwahi kuliongoza taifa hilo la Afrika Magharibi, amekula kiapo mbele maafisa wa Senegal pamoja na wakuu wa nchi kadhaa za Kiafrika.

Faye analenga kuibadilisha Senegal kiuchumi kwa kutumia gesi na mafuta.
Katika hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi, Faye ambaye ni mshirika mkuu wa kiongozi maarufu wa upinzani, Ousmane Sonko, alisema vipaumbele vyake ni maridhiano ya kitaifa, kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha na kupambana na ufisadi.

Lakini changamoto kubwa inayomkabili itakua kukabiliana na viwango vya ukosefu wa ajira,hasa kwa vijana ambao ni karibu asilimia 75 katika nchi yenye watu milioni 18.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kwanini CAF Imemtoza Samuel Eto'o faini...
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limemtoza faini ya Dola...
Read more
“I brought down dollar with my power,...
Read more
INDIA YAPINGA KUHARALISHA MAPENZI YA JINSIA MOJA...
HABARI KUU Mahakama kuu nchini India imekataa kuidhinisha mapenzi ya...
Read more
Eric ten Hag admitted that Brentford win...
While Manchester United's 2-1 victory over Brentford was their first...
Read more
JUDE BELLINGHAM KUKOSA MASHINDANO YA LIGI YA...
MICHEZO Kiungo wa England na timu ya Real Madrid ataukosa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Matajiri wa Chama cha Republican wanamuunga mkono Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kufuatia kesi ya kihistoria dhidi yake na kukutwa na hatia ya uhalifu.

Leave a Reply