Mitandao ya Netblocks na CloudflareRadar inayohusika na ufuatiliaji wa Huduma za Intaneti na Usalama Mtandaoni imesema baadhi ya Nchi Barani Afrika zimepatwa na tatizo la kukatika kwa Huduma za Intaneti, sababu ikidaiwa ni kukatika kwa nyaya katika Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini

Baadhi ya Nchi zilizoripoti kupata shida kwenye mawasiliano ni Tanzania, IvoryCoast ambayo imeripoti kushuka kwa ubora kwa Intaneti hadi 4%, Benin 14% na Ghana kwa 25% huku nchi nyingine zilizopata shida zikiwa ni Afrika Kusini, Nigeria, Liberia, na Burkina Faso

Nchini Tanzania, Mtandao wa Vodacom umekiri kutokea kwa tatizo lililoathiri huduma za M-PESA, Kupiga na Kupokea Simu. Pia, Serikali za Nigeria na Liberia zimesema zimebaini uwepo wa tatizo la Intaneti.

Continue ReadingMitandao ya Netblocks na CloudflareRadar inayohusika na ufuatiliaji wa Huduma za Intaneti na Usalama Mtandaoni imesema baadhi ya Nchi Barani Afrika zimepatwa na tatizo la kukatika kwa Huduma za Intaneti, sababu ikidaiwa ni kukatika kwa nyaya katika Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini