CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania(TALGWU),kimemjia juu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda juu ya matamshi aliyoyatoa dhidi ya Mtumishi wa umma wilayani Longido, kikidai kitendo hicho kinavunja heshima ya mfanyakazi,Kudhalilisha na kuvunja hali na morali ya kufanya kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Leo Mei 28 2024,,Mkuu wa Idara ya habari na Uhusiano wa Kimataifa(TALGWU),Shani Kibwasali amesema mtumishi aliyedhalilishwa na Makonda ni mwanachama wao…