Polisi wa Argentina wanachunguza vitisho vya kifo vilivyotolewa kwa familia ya mshambuliaji Angel Di Maria nyumbani kwao Roasario.

Wafanyakazi kwenye nyumba ya staa huyo mshindi wa Kombe la Dunia na Argentina mwaka 2022, walisema walikutana na ujumbe uliokuwa na vitisho vya vifo kama ataendelea kucheza kwenye moja ya…

Continue ReadingPolisi wa Argentina wanachunguza vitisho vya kifo vilivyotolewa kwa familia ya mshambuliaji Angel Di Maria nyumbani kwao Roasario.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amepiga marufuku safari zote za Nje za Viongozi kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Aprili 1, 2024, lengo likitajwa kuwa ni mpango wa kubana na kupunguza Matumizi ya Serikali yasiyo na ulazima.

Hatua ya Rais inafuatia uwepo wa malalamiko ya Wananchi wanaodai Serikali imekuwa na matumizi makubwa ya Fedha za Walipa Kodi yasiyo na tija, zikiwemo Safari za Mfululizo za Viongozi akiwemo…

Continue ReadingRais wa Nigeria Bola Tinubu amepiga marufuku safari zote za Nje za Viongozi kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Aprili 1, 2024, lengo likitajwa kuwa ni mpango wa kubana na kupunguza Matumizi ya Serikali yasiyo na ulazima.

Mitandao ya Netblocks na CloudflareRadar inayohusika na ufuatiliaji wa Huduma za Intaneti na Usalama Mtandaoni imesema baadhi ya Nchi Barani Afrika zimepatwa na tatizo la kukatika kwa Huduma za Intaneti, sababu ikidaiwa ni kukatika kwa nyaya katika Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini

Baadhi ya Nchi zilizoripoti kupata shida kwenye mawasiliano ni Tanzania, IvoryCoast ambayo imeripoti kushuka kwa ubora kwa Intaneti hadi 4%, Benin 14% na Ghana kwa 25% huku nchi nyingine zilizopata shida zikiwa ni Afrika Kusini, Nigeria, Liberia, na Burkina Faso

Nchini Tanzania, Mtandao wa Vodacom umekiri kutokea kwa tatizo lililoathiri huduma za M-PESA, Kupiga na Kupokea Simu. Pia, Serikali za Nigeria na Liberia zimesema zimebaini uwepo wa tatizo la Intaneti.

Continue ReadingMitandao ya Netblocks na CloudflareRadar inayohusika na ufuatiliaji wa Huduma za Intaneti na Usalama Mtandaoni imesema baadhi ya Nchi Barani Afrika zimepatwa na tatizo la kukatika kwa Huduma za Intaneti, sababu ikidaiwa ni kukatika kwa nyaya katika Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini

Baadhi ya Nchi zilizoripoti kupata shida kwenye mawasiliano ni Tanzania, IvoryCoast ambayo imeripoti kushuka kwa ubora kwa Intaneti hadi 4%, Benin 14% na Ghana kwa 25% huku nchi nyingine zilizopata shida zikiwa ni Afrika Kusini, Nigeria, Liberia, na Burkina Faso

Nchini Tanzania, Mtandao wa Vodacom umekiri kutokea kwa tatizo lililoathiri huduma za M-PESA, Kupiga na Kupokea Simu. Pia, Serikali za Nigeria na Liberia zimesema zimebaini uwepo wa tatizo la Intaneti.

AKILI BANDIA NI HATARI KWA UBINADAMU

NYOTA WETU.

Mmiliki wa mtandao wa X,SpaceX, na Tesla Elon Musk ameonekana kuonyesha wasiw.asi wake juu ya matumizi ya Akili Bandia (Artifical Intelligence (AI)) .

Mapema mwaka huu Musk alionya kuwa teknolojia hiyo inaweza kuleta uharibifu wa ustaarabu.

Bilionea huyo yuko nchini Uingereza kwenye mkutano mkubwa wa AI uliokutanisha mabosi wa teknolojia na Viongozi kutoka pande mbalimbali za Dunia.

Akizungumza na shirika la habari la Sky News ,Musk aliulizwa kama bado anafikiria teknolojia hiyo ni tishio kwa binadamu, naye alijibu kuwa “ni hatari”.

(more…)

Loading

Continue ReadingAKILI BANDIA NI HATARI KWA UBINADAMU