Kiungo wa Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki amekata mzizi wa fitina juu ya mustakabali wake kufuatia taharuki iliyozuka miongoni mwa wapenzi wa soka baada ya posti yake aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii kuzua sintofahamu.
Awali kiungo huyo raia wa Burkina Faso alichapisha taarifa ya kuushukuru uongozi wa klabu hiyo, mashabiki pamoja za wachezaji wenzie kwa mafanikio waliyoyapata katika msimu uliomalizika hali iliyopelekea wengi kudhani…