Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekiri kuwa chama chake cha African National Congress (ANC) kimepata changamoto katika matokeo ya uchaguzi, baada ya chama hicho kupoteza wingi wa kura kwa mara ya kwanza tangu utawala wa kibaguzi kumalizika miaka 30 iliyopita.
Chama cha ANC, ambacho kiliwahi kuongozwa na Nelson Mandela, kilishinda viti 159 katika bunge lenye viti 400 katika uchaguzi wa Jumatano, idadi ya chini kutoka 230 katika bunge lililopita. Ramaphosa…