SIRI YA MICHAEL JACKSON YAFICHUKA

NYOTA WETU

Michael Jackson aliundiwa mfumo wa kucheza ambao ulipingana na nguvu ya mvutano . Ili kutimiza hilo alitengenezewa kiatu maalum na baadaye kupata haki miliki ya kiatu hicho.

Mafanikio ya Michael Jackson ni kama hadithi , ni msanii wa kwanza kushinda tuzo nane za Grammy usiku mmoja; pia ni msanii wa kwanza kuuza nakala zaidi ya milioni moja kwa wiki ya kwanza.

Athari ya uchezaji wake imekuwa ya vizazi kwa vizazi Ulimwengu mzima. Baadhi ya mashabiki wake wamekuwa wakijitahidi kuiga staili zake za uchezaji bila ya kufahamu ,Mfalme wa POP pengine alitumia ufundi wa kisayansi.

Lakini kuna jambo lilishangaza Ulimwengu kwa kucheza akiwa amenyooka na kuinamia mbele akipingana na Nguvu au kani ya mvutano ( gravitational force) alionyesha hivyo kwa mara ya kwanza katika video yake ya mziki ya 1988 “Smooth Criminal “. Katika onyesho hilo Jackson na wachezaji wake wachache wanaegemea mbele kwa kimo cha nyuzi 45,huku migongo imenyooka ,miguu na kushika sakafuni,na kurudi taratibu.

“Haiwezekani kimwili kufanya hivyo ” alisema Daktari wa upasuaji wa neva Dk. Nishant Yagnick ,shabiki wa muda mrefu wa Michael Jackson ambaye anafanya kazi katika Taasisi ya Uzamili ya Elimu ya Tiba na utafiti huko Chandigarh, India.

Unaweza kupinda mgongo kiwango cha juu cha nyuzi 25 hadi 30 kwenda mbele kabla ya kuanguka kifudifudi.

Wacheza Shoo waliofunzwa zaidi wanaweza kuinama kwa kiwango cha juu cha nyuzi 25 au 30 kwa kulalia mbele tena kwa bahati kubwa.

Pamoja na Jackson kuwa na umbo la kipekee katika kucheza,hata yeye hakuweza kufanya hivyo bila ujanja na msaada ,yeye na timu yake walivumbua kiatu maalum ambacho kingemtia nanga kwenye sakafu wakati wa kuinama.

Kiatu hicho chenye haki miliki ya Michael Jackson kina vifaa maalum kwaajili ya kuondoa nguvu ya uvutano na kurahisisha uchezaji ule na pia kuzuia kuanguka.

Viatu hivyo vilipewa haki miliki Octoba 26,1993 ,vina sehemu ya kisigino iliyoundwa maalumu ambayo inaweza kuunganishwa kwa urahisi na kitu kama vile jukwaa au sakafu.

Kabla ya kucheza kwa kutumia viatu hivyo unatakiwa kuwa na mazoezi ya kutosha pia na daktari wa mziki.

(more…)

Loading

Continue ReadingSIRI YA MICHAEL JACKSON YAFICHUKA