Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini – TMA, imetoa angalizo kwa wakazi wanaoishi ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam, kwamba kuna uwezekano wa kukutana na hali mbaya ya hewa kwa siku tano na Mvua za siku tatu mfululizo.
Kupitia utabiri wake wa hali ya hewa, TMA imeeleza kuwa, maeneo mengine yanatakayokumbwa na hali hiyo ni mikoa ya Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi, Mtwara pamoja na visiwa…