Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini – TMA, imetoa angalizo kwa wakazi wanaoishi ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam, kwamba kuna uwezekano wa kukutana na hali mbaya ya hewa kwa siku tano na Mvua za siku tatu mfululizo.

Kupitia utabiri wake wa hali ya hewa, TMA imeeleza kuwa, maeneo mengine yanatakayokumbwa na hali hiyo ni mikoa ya Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi, Mtwara pamoja na visiwa…

Continue ReadingMamlaka ya Hali ya Hewa Nchini – TMA, imetoa angalizo kwa wakazi wanaoishi ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam, kwamba kuna uwezekano wa kukutana na hali mbaya ya hewa kwa siku tano na Mvua za siku tatu mfululizo.

MFAHAMU MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA
DR.PHILIPO ISDORY MPANGO.

Amezaliwa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu. Dk Mpango alizaliwa hapohapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi – Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.

Historia na elimu

Dk Philip Mpango alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano, ameteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Magufuli. Ni mbunge wa kuteuliwa.

Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi. Hata hivyo, hadi sasa taarifa zake za elimu ya msingi, sekondari na shahada za awali za chuo kikuu hazijapatikana naye amekuwa vikaoni Dodoma muda mrefu na alishindwa kuzitoa kwa wakati.

Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alikuwa akifundisha “Microeconomics”, “Macroeconomics” (kwa mwaka wa pili) na “Public Finance” kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili.

Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais. Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.

Hayati John Pombe Magufuli alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Nguvu

Kwanza, Dk Mpango ni kiongozi mwenye msimamo thabiti. Baadhi ya watendaji ambao wamewahi kufanya kazi chini yake kwenye ofisi ya Rais wanamuelezea kama mtu anayetaka waliomzunguka wazungumze kwa takwimu na ushahidi hasa katika masuala ya uchumi. Msimamo huo pia aliuonyesha alipokuwa mtaalamu wa Benki ya Dunia. Hakuwa mwoga kuieleza ukweli Serikali pale ambako ilikuwa haifanyi vizuri.

Mathalan, wakati wasomi wengi wa uchumi wakiwa wanapiga kelele za kuisifia Serikali juu ya ukuaji wa uchumi miaka ya mwanzoni ya 2000, Dk Mpango alieleza wazi kuwa lengo hilo la kukuza uchumi kwa asilimia 5.9 haliwezi kufikiwa kwa sababu katika miaka minne iliyopita, Serikali ilishindwa kulifikia.

Alisema: “Angalia kwa miaka minne hadi mitano iliyopita ambayo tulikuwa na sera nzuri za kibajeti, hakuna mwaka ambao ukuaji huo ulifikiwa, hizo ni dalili tosha kwamba hali hiyohiyo ndiyo itajitokeza mwaka huu.”

Misimamo ya namna hii ni nadra kwa wasomi wa ngazi yake walio wengi, ambao hubakia kusifia kila kinachotendwa na Serikali ilimradi kwa kutegemea siku moja watateuliwa kushikilia nyadhifa kubwa. Ushahidi wa msimamo wa Dk Mpango pia umeelezwa na baadhi ya wanafunzi wake aliowafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wengine ni wahadhiri katika chuo hicho hivi sasa. Mwanafunzi wake amenieleza kuwa kama kuna mwalimu ambaye wanafunzi wa uchumi walikuwa wanampenda na kumheshimu ni daktari huyu. Pia anasema kama kuna mwalimu ambaye walikuwa wanamuogopa kwa misimamo yake ni huyu.

Nimeambiwa wakati wote alitaka wanafunzi wake waenende na miiko ya kitaaluma na hakuchelewa kuwa rafiki wa yeyote pale anapofanya vizuri.

Pili, ni kiongozi mwenye dira na maono mapana, ni mtendaji anayeweza kusimamia jambo alilokabidhiwa na likafanikiwa. Alipoteuliwa kuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, ndani ya mwezi mmoja ukusanyaji wa mapato wa taasisi hiyo ulivunja rekodi. Kwa mara ya kwanza TRA ilikusanya zaidi ya Sh1.4 trilioni kwa mkupuo. Rais JPM alijitokeza na kumpongeza kwa hatua hiyo na muda mfupi baadaye akamkabidhi Wizara ya Fedha.

Bila shaka hapa tunaweza kupata jambo la nne linalomuongezea nguvu, suala la kujua vyanzo vya umaskini wa Taifa na wapi linafanya makosa kwenye uchumi, ukusanyaji wa mapato na uongezaji wa vyanzo vya mapato. Haya, hajayaokota tu barabarani, ameyaishi tokea akiwa mwalimu wa chuo kikuu na baadaye kufanya kazi kubwa Benki ya Dunia kabla ya kuajiriwa kusaidia mambo ya kiuchumi akifanya kazi kwenye Ofisi ya Rais.

Katika moja ya andiko lake kwenye kitabu cha mwaka 2008 kilichoshirikisha wataalamu wa Benki ya Dunia na ile ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kiitwacho “Sustaining and Sharing Economic Growth in Tanzania” (Ukuaji wa Uchumi Endelevu na Shirikishi Tanzania – kwa tafsiri yangu) na kuhaririwa na Robert J. Utz, Dk Mpango amefafanua ukuaji wa uchumi kwa mujibu wa tofauti za kikanda hapa Tanzania akionyesha tofauti ya vipato katika mikoa na kanda za Tanzania, namna ambavyo rasilimali za Taifa zinagawanywa bila usawa katika kanda na mikoa, akieleza vikwazo vikuu vya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu na kupendekeza hatua za kimikoa na kikanda zinazopaswa kuchukuliwa ili kuufanya uchumi wa Tanzania upae.

Ukilisoma andiko hilo, unaweza kugundua kuwa nchi inao wataalamu na wasomi waliobobea na wenye uwezo mkubwa wa kuyajua matatizo ya uchumi na njia za kuyatatua lakini unaweza kujisikia vibaya kwamba wamekuwa hawasikilizwi na Serikali haina muda na maandiko kama haya ambayo yanatumiwa na nchi nyingine kujikwamua kiuchumi. Ubobezi na ujuzi wake kwa uchumi wa chini na juu wa wananchi na kujua matatizo na hatua za kuchukua ni kigezo tosha kitakachomsaidia daktari huyu kuchukua hatua za kiuchumi za kulivusha Taifa kwakuwa sasa watanzania tumejua kuitumia dhahabu iliyofichika kwenye mchanga.

Siasa

Kwa kiasi kikubwa Dr Mpango hakuwahi kuzama kwenye siasa Moja kwa Moja kiongozi huyu hata siku moja hakuwahi kuwa na ndoto za kuwa mwanasiasa wala hakuwahi kutamani na kufikiria nyadhifa za juu .

..

Continue ReadingMFAHAMU MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA