HABARI KUU Mamlaka ya Uchina inachunguza baada ya video iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha mfanyakazi kutoka Tsingtao akikojoa kwenye tanki ,linaloaminika kuwa na viambato vya bia. Klipu hiyo iliyotazamwa na mamilioni ya…
MICHEZO Kuelekea michezo ya hatua ya robo fainali ya kombe la Afrika (AFL) kesho kati ya Simba na Al Ahly, katika dimba la Cairo ,imebainika sasa kuwa goli la ugenini…
MASTORI Mchambuzi Garry Neville "Chelsea imeonyesha dalili za kwa namna gani watakuwa hapo mbeleni . Bado wana matatizo kwenye ushambuliaji, bado hawajampata Mshambuliaji bora. "Unaweza kuona sehemu ya kiungo na…
HABARI KUU Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliokutana hivi leo tarehe 22 Oktoba, 2023 mjini Dodoma,katika kikao chake maalumu, chini ya Mwenyekiti wa CCM ,ndg Dkt. SAMIA SULUHU…
MICHEZO Nyota wa Real Madrid ,Vinicius Junior ametoa pongezi kwa klabu ya Seville kwa kuchukua kwa hatua za haraka za kumtoa uwanjani na kuripoti kwa mamlaka shabiki wake kwa madai…
Kumekuwa na sintofahamu nchini Kenya baada ya Rais wa Angola Joâo Lourenćo kutokuhudhuria sherehe za Mashujaa Day Nchini Kenya kama ilivyotarajiwa licha ya kuwasili nchini humo.
Mtandao wa “Daily Nation ” umeripotiwa kuwa Waziri Mkuu, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya,Musalia Mudavadi ,wakati akimpokea mgeni huyo aliyeambatana na mkewe Ana Dias Lourenço,alidokeza kuwa ndiye aliyealikwa kuwa mgeni wa heshima katika sherehe hizo.
Rais huyo wa Angola 🇦🇴 aliwasili Kenya siku ya Alhamisi ambapo ilitarajiwa afike Kericho ambako ndiko sherehe hizo zilifanyika kitaifa, huku akitarajiwa kuwa mgeni wa heshima kwa mujibu wa mawasiliano rasmi kati ya Kenya na Angola 🇦🇴.
Hata hivyo jana Ijumaa Oktoba 20,2023 katika programu rasmi ya “Mashujaa Day ” haikuorodhesha uwepo wa Rais Lourenço kama mgeni rasmi ,badala yake aliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Balozi António Tete.
Katika hotuba yake ,Balozi António Tete amesema kutokuwepo kwa Rais Lourenço kumetokana na “sababu zisizotarajiwa” na hivyo kuwaomba radhi Wakenya kwa niaba ya Rais wake.
“Kwa niaba ya Rais Joáo Lourenço kwanza ningependa kuomba radhi kwa kutokuhudhuria sherehe hizi. Angependa kuwa pamoja nanyi lakini kwasababu ya sababu zisizotarajiwa, hakufika Kericho
“Hata hivyo,anawatakia kheri mnaposheherekea siku hii ya leo muhimu, pia anawashukru kwa mapokezi mnayotupa tunapokuja Kenya 🇰🇪 “
Amesema balozi Tete
Katika hotuba yake wakati wa sherehe hizo, Rais William Ruto amesema kuwa Rais Lourenço bado yuko nchini humo na kwamba atakuwa na ziara ya kiserikali leo jumamosi.
“Tunapozungumza sasa, Rais Joáo Lourenço wa Angola bado yuko Kenya 🇰🇪, na atakaribishwa katika ziara ya kikazi kuanzia kesho jumamosi “.
Rais Samia Suluhu Hassan ameibuka tishio kwa vyama vya upinzani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa 2025 kutokana na umati mkubwa anaovuta kwenye ziara zake akiwa kwenye mikoa mbalimbali.
Popote aendako kwenye ziara zake kwenye mikoa mbalimbali, Rais Samia amekuwa akilakiwa na umati mkubwa wa watu jambo ambalo sasa ni nyota ya kijani kwake kuelekea Uchaguzi wa 2025 anaweza kuibuka kidedea mapema.
Kada mbalimbali za wananchi,ikiwemo ya vijana madereva bodaboda ,kina mama lishe, wakulima ,wavuvi,wafugaji ,wafanyabiashara na wananchi wa kawaida wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kumlaki Rais ,kitu ambacho akikuwahi kutokea.
Ingawa bado ni mapema mno na Rais Samia bado hajatangaza nia yake ya kugombea urais 2025, lakini ni wazi Rais Samia kwasasa anaonekana ni mwanasiasa mwenye ushawishi zaidi kwasasa nchini na ni turufu kubwa ya uchaguzi mkuu.
Katika ziara zake za hivi karibuni kwenye mikoa ya kusini na katikati mwa nchi amejizolea maelfu ya watu hasa mkoa wa Singida ambayo ilionekana ni ngome ya Lissu lakini imekuwa tofauti kwani amepata watu wengi .