Dar es salaam.
Klabu ya #Yanga imefungiwa kusajili baada ya kushindwa kwenye kesi na mchezaji wake wa zamani Gael Bigirimana. Yanga ilipewa siku 45 kuhakikisha imemlipa mchezaji huyo raia wa Burundi malipo yake ya ada ya usajili.
Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini haikutekeleza hukumu hiyo .
Wakati FIFA inaifungia klabu hiyo kwa kutofanya uamisho wa wachezaji wa kimataifa,shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limeifungia klabu hiyo kufanya usajili au uamisho wa ndani.
TFF inazikumbusha klabu ,kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili iwapo klabu inataka kuvunja mkataba na mchezaji au kocha inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu .