Gabon
Katika hali isio ya kutegemewa,majeshi ya Gabon yamefanikiwa kumwangusha Ali Odhimba Bongo Rais wa nchi hiyo ambaye ametawala tokea 2009 mpaka leo. ALI BONGO mtoto wa Kanali Omar Bongo ambaye aliitawala nchi hiyo toka uhuru mwaka 1967 mpaka alipofikwa na umauti mnamo mwaka 2009.
“Tumevunja Bunge,Serikali na Mahakama. Hakuna mhimili wowote utakaofanya kazi kuanzia sasa.Jeshi litaongoza nchi kwa kipindi cha mpito hadi hali itakapotulia.Tumefanya hivi kulinda watu wetu na amani yetu” Taarifa ya jeshi imeeleza.
Ikiwa ni tu jana ,Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo (CGE) ilitangaza Rais Ali Bongo anayegombea kwa awamu ya 3 amepata kura 64.2% huku mpinzani wake mkuu Profesa Albert Ondo Ossa akioata 30.7%. Baada ya matokeo kutangazwa ,watu mamia kwa maelfu ya raia waliandamana kwenye sehemu mbalimbali ya nchi hiyo.
Baada ya mapinduzi haya ,familia ya Bongo inahitimisha miaka 57 ya kuliongoza taifa la pembe ya Magharibi mwa Afrika lenye utajiri wa mafuta na gesi, taifa ambalo ni koloni la zamani la Ufaransa.
Familia ya Bongo inashutumiwa kwa Matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma.Mwaka 2019 ndugu wa Rais Bongo ,ambao ni Omar Denis Bongo na Paskalina Bongo walituhumiwa kupokea rushwa ya $85 milioni hili kuisaidia kampuni ya Ufaransa kuchimba mafuta nchini humo na pia sehemu ya utawala wa Bongo umekuwa wa upendeleo hasa ndugu na watu wa karibu wa familia hiyo kupewa vyeo ndani ya serikali.
Haya ni mapinduzi ya 6 kwa siku za hivi karibuni kwenye nchi zilizopo kwenye jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi yaani ECOWAS, ambapo mapinduzi yalianzia Burkina Faso,Mali,Niger,Chad,Guinea na hatimaye Gabon. Pamoja na juhudi za jumuiya ya Ecowas kupinga vikali mapinduzi ya kijeshi,raia wamekuwa upande wa jeshi na huku ikitajwa ni Urusi ina mkono wake kuhakikisha Makoloni ya Ufaransa yote inayanyakua.