JE KUONEANA WIVU NI SEHEMU YA MAPENZI?

0:00

Makala Fupi

Mapenzi yananoga wivu unapokuwa ndani yake. Ukitathimini kwa harakaharaka ,unaweza kusema kama hakuna wivu ,hakuna mapenzi. Inapotokea mpenzi wako, hata ufanye nini hakuonei wivu,bila Shaka hata wewe utahisi kuna tatizo.

Unatamani kale “kawivu” kidogo ili ujisikie unapendwa. Maana,tafsiri nyingine ya mtu asiyekuwa na wivu,huwa ni ile ya “wewe fanya yako, na mimi nifanye yangu,tusiingiliane”.

Wivu unapozidi kipimo ,nalo huwa ni tatizo lingine.Tunakubaliana hakuna ambaye atafurahia pindi asikiapo mwenzake amemsaliti. Ndiyo maana wapendanao hutumia nguvu nyingi sana kuhakikisha tu mwenzake hamsaliti.

Wapo ambao wanadiriki hata kuwawekea ulinzi wenza wao ili kuhakikisha kwamba kila kitakachofanywa na mpenzi wake anakijua . Kila eneo atakapokuwa mpenzi wake kunakuwa na watu wanaofikisha habari kama zilivyo.

Kundi la wanaume au wanawake wa aina hiyo ndiyo wale wanaokosa ustahimilivu akiona mpenzi wake amesimama na mtu tu barabarani,hana imani. Anatamani kujua wanazungumza nini ? Mpenzi wake akichelewa kurudi nyumbani, anatilia Shaka.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MAMA NA WANAWE PACHA WAFA MAJI MTO...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
BENZEMA ATAJWA KWENYE UGAIDI KISA HIKI ...
MICHEZO Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa ,Gerald Damarnin...
Read more
SABABU ZIWA TANGANYIKA KUFUNGWA MIEZI MITATU...
HABARI KUU Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza...
Read more
Je Mwanamke anahitaji Muda Gani Kufika Kileleni?
Moja ya changamoto inayowasumbua wanaume wengi mno ni kuwa na...
Read more
Tragic Road Accident in Garissa Leaves 10...
A road accident in the Katumba area along the Garissa-Nairobi...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply