NYOTA NJEMA ILIVYOZIMA YA MOHBAD

0:00

NYOTA WETU

Mwaka 2020 kijana Ilerioluwa Oladinaji Aloba alijiunga na Marlian Music ambayo inamilikiwa na mwanamziki Naira Marley, baadae miaka miwili Mohbad alijiondoa kwenye hiyo record lebel huku ikitajwa mahusiano mabovu na bosi wake.

Mohbad ambaye alizaliwa Juni 8,1996 na kufa kwa kifo cha kushitukiza Septemba 12,2023 alizikonga nyota za mashabiki baada ya kutoa EP (Extended Playlist) mwaka 2022 ambayo ilimpa mashabiki wengi na kumtambulisha kama Mwanamziki mwenye kipaji kikubwa nchini Nigeria hasa kwenye jiji la Lagos.

Mohbad baada ya kushindwa kuendelea na Naira Marley alianza kuingia kwenye misukosuko ya kimaisha na huku mara kadhaa alikuwa akilalamika kutishiwa maisha na hivi karibuni kabla ya kifo chake inatajwa alikutana na mlinzi Sam Rally ambaye ni rafiki wa karibu wa Naira Marley .

Mohbad baada ya kukutana na Sam Rally ambaye anatajwa kumiliki genge la wahuni hapo Nigeria, akilalamika kuwa alikuwa amepuliziwa dawa ambayo ilikuwa ikimzoofisha afya yake.

Mohbad ambaye alitoa vibao kama peace,Beast and Peace na Ask about me alifariki kwa kifo ambacho kimezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, wengi hasa wanaigeria wakitaja amenyongwa na wengine wakitaja alichomwa na sindano yenye sumu. Baada ya kifo chake ,alizikwa haraka haraka huku ikionesha alivunjwa shingo. Mamlaka nchini Nigeria, kwenye jiji la Lagos limelazimika kuufukua mwili wa msanii huyo nyota kwaajili ya uchunguzi zaidi.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  SITI BINTI SAAD: JOHARI LA MUZIKI WA TAARABU ZANZIBAR
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading