MFAHAMU OSMAN BEY KIPENZI CHA WAPENDA FILAMU

0:00

NYOTA WETU

Burack Ozcivit wengi mnamfahamu kama Osman Bey kama jina lake la uigizaji lilivyo,ndoto zake zilikuwa ni kuwa mwanamitindo wakati akiwa ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Marmara huko Istanbul. Mwaka 2003 nyota yake ilianza kung’ara kwa kuwa mwanamitindo wa uturuki na miaka miwili baadae 2005 alitambuliwa kwa kushika nafasi namba 5 kwa kuwa mwanamitindo bora Duniani.

Osman Bey alikulia Istinye Jiji la Istanbul, alizaliwa Desemba 24,1984. Mwaka 2006 akiwa kijana mdogo tena wa chuo alichaguliwa kushiriki kwenye Tamthilia ya Eksi 18 ambapo alifanya vizuri na kuwavutia sana waongozaji wa filamu nchini humo.

Msanii huyu alihitimu chuo akiwa na shahada ya upigaji wa picha na uongozaji. Tamthilia ya Calikusu ilianza kumuweka kwenye njia ya umaarufu 2013-2016 moja kati ya kazi nzuri iliyomtambulisha vyema ikiwemo hapa Tanzania ni Tamthilia ya Kara Sevda.

Alijulikana kama Macchoglu bali Bey kwenye Tamthilia pendwa ya Muhtezem Yuzlil ,wengi wakihifahamu kama SULTAN.

Kwa mujibu wa chapisho la Businessdor.com katika chapisho lake la mwezi February 20,2023 walimtaja kama msanii mkubwa anayelipwa pesa nyingi kwenye matangazo ya biashara.

Mke wake ni Fahriye Evcen ni mjerumani aliyefunga nae ndoa mwaka 2017 ,na kujaliwa watoto wawili wa kiume Karan Kerem. 2023,kwa mujibu wa medium.com inatajwa pia mke wa Osman Bey naye anafanya matangazo kwa bei mbaya.

Osman Bey anatajwa ana ukwasi wa bilioni 18 za kitanzania.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SABABU VINICIUS JR KUBAGULIWA ZAIDI VIWANJANI ...
NYOTA WETU Winga wa Brazil na Real Madrid Vinicius Jr...
Read more
Issa Hayatou Afariki Dunia
Rais wa zamani wa shirikisho la soka barani Afrika CAF...
Read more
WAZIRI MKUU APATA KAZI YA UTANGAZAJI ...
NYOTA WETU
See also  MWANAUME AWAPA WANAWAKE WATANO UJAUZITO KWA MARA MOJA
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson...
Read more
TABIA 10 ZINAZOFANYA WANANDOA KUISHI KWENYE NDOA...
MAPENZI Kuzeeshana kwenye ndoa ni jambo ambalo kila mwanandoa analitamani...
Read more
HOW TO HANDLE A MAN AND MAKE...
LOVE ❤ 1. Respect him, honour him, submit to his...
Read more

Leave a Reply