DON 3 KUACHILIWA BILA MKALI SHAHRUKH KHAN

0:00

Nyota Wetu

Hii ni habari kama isiyopendeza kwa mashabiki wa nguli SHAHRUKH KHAN ambao pia wanapenda kumuona bado kwenye mfululizo wa movie za Don.

Mashabiki wengi hawakuunga mkono ujio wa mpya wa Don 3 bila ya uwepo wa staa huyo,tulio wengi hatujajua ni sababu zipi zimemfanya nyota huyo ajiondoe kwenye Don pamoja na umaarufu wake mkubwa kuifanya movie hii kuwa kubwa.

Mkurugenzi wa Filamu za Don ambaye pia ni muigizaji Farhan Akhtar amefunguka kuhusu kujiondoa kwa SHAHRUKH KHAN kwenye mfululizo wa Filamu maarufu ya DON 3 ,akitaja “tofauti za kiubunifu”kama sababu ya wawili hao kusitisha ushirikiano wao katika awamu ya tatu ijayo,ambayo sasa inamshirikisha Ranveern Singh kama mhusika mkuu.

SHAHRUKH KHAN

“Siko katika nafasi ya kuchukua nafasi ya mtu yeyote, haya ni mambo tuliojadili miaka mingi . Nilitaka nichukue mwelekeo fulani na hadithi ,lakini kwa njia fulani hatukuweza kupata msingi wa kawaida. Tumeachana tu tukijua labda ni bora zaidi. Hivyo hapa ndipo ilipo”

Akhtar alisema katika mahojiano na chapisho la Marekani la Variety.

Mkurugenzi huyo wa Dil Chahata Hai pia alisema kuwa anafurahi kufanya kazi na Ranveern Singh katika awamu ya tatu ya franchise.

“Nimefurahishwa sana na Ranveern kwenye bodi.Amejadiliwa sana na yuko tayari kuwa Don mpya. Ni filamu kubwa tu kwa mtazamo wa mwigizaji”.

Ranveern Singh

Filamu hiyo ipo chini ya kampuni ya uzalishaji wa filamu ya Excel Entertainment ya Farhan Akhtar na Ritesh Sidhwan na tayari ilimzindua Ranveern kama sura mpya ya Don kupitia kionjo cha tangazo la Don 3 mwezi uliopita kilichosomeka “Enzi mpya imeanza”.

Movie inatarajia kutolewa 2025.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Sea water boat reflection red vehicle
Nullam eget felis eget nunc lobortis mattis. Pharetra diam...
Read more
TABIA 10 AMBAZO KILA MWANAUME ANAZO
LOVE TIPS ❤
See also  WACHEKESHAJI WAWILI MBARONI
1. Mwanaume ni mtu mwenye sifa kama...
Read more
NASTY C TIME IS OVER
CELEBRITIES "At some point in time I was the best...
Read more
ORODHA YA WATU 20 MATAJIRI ZAIDI BARANI...
MAKALA Aliko Dangote (Nigeria) – $13.9b Johann Rupert (S. Africa) –...
Read more
Victor Osimhen's successor as African Footballer of...
The Confederation of African Football (CAF) says the prestigious CAF...
Read more

Leave a Reply