BENZEMA ATISHIWA TENA

0:00

MICHEZO

Kufuatia shutuma za Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Gerald Darmanin, kuwa Karim Benzema “ana uhusiano ” na kundi la kigaidi la Muslims Brotherhood, seneta wa Ufaransa Valerie Boyer ,ameibuka na kutoa kauli tata dhidi ya Mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid.

Kupitia taarifa kwenye vyombo vya habari, Seneta huyo ametaka hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya Benzema, ikiwa tuhuma za kujihusisha na kundi la “Muslims Brotherhood ” zitathibitishwa kutoka kwa Waziri huyo wa mambo ya ndani.

Kwenye taarifa hiyo ,Seneta Boyer alisema,

“Kama kauli za Waziri wa Mambo ya Ndani ni kweli, lazima Karim Benzema awekewe vikwazo “.

“Kwanza Benzema apokonywe tuzo yake ya Ballon dOr,lakini pia,ni lazima mchezaji huyo avuliwe uraia wa Ufaransa. Hatuwezi kukubali Mfaransa mwenye uraia pacha ,na kujulikana kimataifa, atuvunjie heshima na kuisaliti nchi kiasi hiki”.

Mjjadala na tuhuma hizo imeibuka baada ya Benzema kukaa kimya kwenye shambulizi la kigaidi lililohusisha mauaji ya mwalimu Ufaransa nje ya mji kidogo wa Paris, huku siku chache baada ya tukio hilo,Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutoa pole kwa raia wa Palestine huku akitaka haki itendeke.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Uchambuzi: 𝗞𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗨𝗦𝗔𝗝𝗜𝗟𝗜 WA Y𝗔𝗡𝗚𝗔
"𝗬𝗮𝗻𝗴𝗮 𝗶𝗻𝗮𝘀𝗮𝗷𝗶𝗹𝗶 𝗸𝗶𝗺𝗮𝗵𝗲𝘀𝗮𝗯𝘂 𝘀𝗮𝗻𝗮 ..Kuna wakati nilikuwa najiuliza, hivi vilabu...
Read more
SERIKALI YAWAITA WAWEKEZAJI KWENYE SGR
HABARI KUU Shirika la Reli Tanzania (TRC) limechukua hatua muhimu...
Read more
TUNDU LISSU AMSHTUKIA MBOWE KUELEKEA 2025
HABARI KUU Baada ya Lissu kutangaza jukwaani kuwa rushwa imekithiri...
Read more
TABIA 23 ZA MWANAMKE MPUMBAVU ...
MASTORI
See also  HOW TO MAKE YOUR WIFE RESPECT YOU IN THE MARRIAGE
1. Ni mbishi na hana utii kwa mume wake 2.Ni...
Read more
FLAVIANA MATATA AFUNGUKA SABABU ZA KUTOPENDA KUOLEWA
NYOTA WETU Sina ndoa wala mtoto sijisikii kwasasa, naogopa kuwa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply