PAPA ATEUA MAPADRI HAWA KUWA MAASKOFU

0:00

HABARI KUU

Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani, Papa Francisco amewateuwa mapadri wawili kuwa maaskofu kwenye majimbo mawili ya kikatoliki ya Njombe na Bukoba.

EUSEBIO KYANDO

Maaskofu hao wateule ni pamoja na; Padri Jovitus Mwijage kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba na Padri Eusebio Kyando kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe .

Katika taarifa iliochapishwa na Vatican inasema Papa Francisco amemteua Padri Eusebio Kyando kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa msimamizi wa kiroho wa jimbo hilo.

Jimbo Katoliki la Njombe limekuwa wazi kwa muda mrefu kufuatia kifo cha Mhashamu Askofu Alfred Maruma na kwa upande wa jimbo la Bukoba Mhashamu Askofu Desderius Rwoma alistaafu kwa mujibu wa sheria za kanisa katoliki.

JOVITUS MWIJAGE

Hii ni mara ya kwanza kwa kanisa katoliki kupata teuzi mbili za maaskofu kwa wakati mmoja kwa miaka ya hivi karibuni kutoka kwa Baba Mtakatifu.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KASI YA ONGEZEKO LA WAJANE YASHTUA HADHARI...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
MANCHESTER CITY YAICHAPA MANCHESTER UNITED
MICHEZO Manchester City wameitembezea kichapo cha 3-1 majirani zao wa...
Read more
BUSINESS MARKETING RESEARCH
What Is Market Research? The term market research refers to the...
Read more
JESHI LA POLISI LAMTIA NGUVUNI ALIYESAMBAZA TAARIFA...
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata...
Read more
BODABODA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA ABIRIA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  ATEKWA NA WENZAKE KWA KUWATAPELI MADAWA YA KULEVYA

Leave a Reply