HABARI KUU
Waziri Mkuu wa Iceland Katrin Jakobsdottir ,leo anaungana na maelfu ya wanawake kuandamana kudai malipo sawa pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia.
Maandamano hayo yanalenga kuongeza ufahamu juu ya ubaguzi wa kwenye malipo pamoja na ukatili wa kijinsia.
Akizungumza na vyombo vya habari Waziri Mkuu amesema
“Sitafanya kazi leo ,kama ninavyotegemea wanawake wengine wote kwenye Baraza la Mawaziri wote kutofanya kazi.”.
“Nimeamua kutokuwa na Mkutano kwenye Baraza kesho ,na Bungeni maswali yote yatajibiwa na Mawaziri wanaume”.
Kupitia tovuti yao waandaaji wa maandamano hayo waliwahimiza wanawake wote nchini humo wakiwemo wahamiaji kutofanya kazi kwa siku ya leo ,iwe ni za kulipwa au za kutolipwa ikiwemo kazi za ndani.
Kwa siku nzima wanawake watagoma hili kuonyesha umuhimu wa mchango wao kwenye jamii.
Pamoja na kuwa na Maendeleo, wanawake katika kazi nchini humo hulipwa karibu 20% chini ya wanaume.
Vilevile idadi kubwa ya wanawake nchini humo unyanyasika kijinsia nchini humo.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.