HABARI KUU
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Godbless Lema kupitia ukurasa wake wa Instagram, amemsihi Rais Samia Suluhu Hassan kujihadhari na wapambe na machawa.
“Mheshimiwa nakusalimu. Wewe ni Rais wa nchi,ikiwa utaongezewa na Urais wa taifa kama Marekani halafu utajiri wako ukawa kama wa Elon Musk na Jeff Benzos ,ukapata na fursa ya kujenga nyumba ya kisasa katika sayari ya Mars ambako bomu la Nyuklia haliwezi kuathiri .
Pia watoto wako wote wakamiliki majengo mengi kama ulivyo mji wa New York na Paris na Kisha wakawa wamiliki wa share za mabenki makubwa Duniani, unafikiri hayo yanatosha kuwa mafanikio kama kuishi kwako kunaongeza huzuni kwa maisha ya watu?
Maisha yanaenda kwa kasi sana, unajua ni juzi tu Magufuli ,Mkapa na Nyerere walikuwepo kabisa na walikuwa na wapambe wengi sana. Jiadhari na wapambe na machawa nafikiri wao kwasasa wanaweza kuwa mlango wa Jehanum kuliko dhambi nyingine yeyote, wako ambitious na lunch,school fees za watoto wao kwa gharama yoyote ile na urban lifestyle kuliko wema “
Ameandika Godbless Lema.