ZIARA YA MFALME KENYA YAIBUA MAZITO

0:00

HABARI KUU.

Wazee wa jamii ya Nandi nchini Kenya wametoa wito kwa kurudisha fuvu la Koitalel Arap Samoei ,chifu pamoja na kiongozi wa kiroho na kijeshi aliyeuawa na Waingereza mwaka 1905.

Matakwa hayo mapya yanakuja siku chache kabla ya ziara ya mfalme Charles III nchini Kenya Oktoba 30,2023.

Samoei aliyeongoza upinzani mkali dhidi ya wakoloni ,aliuawa na mwanajeshi wa Uingereza kanali Richard Meirnertzehagen ,baada ya kuwalaghai Samoei na Viongozi wengine wa Nandi wa kuhudhuria mkutano wa mapatano.

Kulingana na gazeti la Daily Nation la nchini Kenya, wazee hao pia wanataka kurejeshwa kwa vitu vyao vya kitamaduni vilivyoibwa na kufidiwa kwa ukatili waliofanyiwa jamii wakati wa utawala wa wakoloni .ikiwa ni pamoja na mauaji ,kuwekwa kizuizini na kuwahamisha watu wa jamii ya Nandi kwa nguvu.

Fuvu la Koitalel Arap Samoei inasadikika kuwa katika mkusanyiko wa makumbusho mahali fulani nchini Uingereza.

Wazee wa Nandi mara kwa mara wamekuwa wakiomba kurejeshwa kwa mabaki hayo ya Samuel.

“Tunamsihi Mfalme Charles, tunahitaji kupata fuvu hilo lirudishwe Nandi tufanye mazishi ya heshima.

David Samoei aliliambia shirika la utangazaji la KTN mapema mwaka huu.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

LVMH's Arnault, Red Bull in talks to...
PARIS, - French billionaire and LVMH(LVMH.PA), opens new tab chairman...
Read more
Matapeli Wa Mtandaoni Wakamatwa Tanga
Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga limefanikiwa kuwakamata watu watano...
Read more
Probierz praises Poland's resilience in thrilling 3-3...
Poland coach Michal Probierz praised his team's resilience and attacking...
Read more
Cristiano Ronaldo etched his name in the...
In a groundbreaking achievement, football legend Cristiano Ronaldo has etched...
Read more
RAHEEM STERLING AKANUSHA TETESI ZA KWENDA SAUDIA...
MICHEZO
See also  SUALA LA THABO MBEKI LILIVYO KWASASA
Kiungo Mshambuliaji wa Chelsea, Raheem Sterling haonekani kupendezwa na...
Read more

Leave a Reply