HABARI KUU
Related Content
Taarifa kutokea ofisi ya Rais wa Austria imesema hali ya Rais Alexander van Der Bellen inaendelea vizuri baada ya kung’atwa na mbwa wa Rais wa Moldova
wakati wa ziara ya kikazi.
Rais huyo aling’atwa mkono baada ya kuinama akijaribu kumgusa mbwa huyo aitwaye Codrut .
Rais Maia Sandu wa Moldova ameomba msamaha kwa kitendo hicho cha mbwa wake kuharibu itifaki za kimataifa.

Vilevile anasema Condrut alishikwa na woga baada ya kuzungukwa na umati mkubwa wa watu wengi.