AFARIKI AKIFANYA UPASUAJI WA KUONGEZA MAKALIO

0:00

HABARI KUU

Maofisa wa Uingereza na Uturuki watakutana kujadiliana kuhusu mfumo wa udhibiti kufuatia kifo cha Mwanamke mmoja mwaka 2019 kilichotokea katika upasuaji wa kuongeza makalio.

Melissa Kerr alifariki Dunia jijini Istanbul mara baada ya kufanyiwa upasuaji uliohusisha kukusanya mafuta na kuyaweka kwenye makalio yake.

Kifo cha Melissa (31) kilitokana na mafuta aliyochomwa kwenye makalio aliyochomwa kuingia kwenye mishipa na baadaye kwenda kuziba ateri ya mapafu.

Sababu ya kifo chake ilirekodiwa kuwa kuwa ni kuziba kwa ghafla kwa mishipa ya damu kulikotokana na kuwekewa mafuta. Huku sababu kuu ikiwa ni upasuaji wa urembo.

Maafisa hao wanaeleza kuwa Melissa hakuwa amepewa taarifa za kutosha kuhusiana na hatari za upasuaji huo ikiwemo kiwango cha vifo.

Vilevile wamesema yawezekana hakuna kabisa udhibiti au upo kidogo sana kuhusiana na upasuaji wa urembo.

Wizara ya Mambo ya nje ya Nchi ya Uingereza imeeleza inazo taarifa hizo zaidi ya raia wake 25 walipoteza maisha nchini Uturuki tangu January 2019 baada ya kufanyiwa upasuaji wa aina mbalimbali.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

DNA test confirms that the three children...
DNA tests have revealed that Nigerian soccer star Kayode Olanrewaju...
Read more
REAL MADRID MABINGWA WA SPANISH SUPER CUP...
MICHEZO. Real Madrid imetwaa Ubingwa wa Spanish Super Cup 2024...
Read more
ZIDANE AONYWA NA MPANGO WAKE WA KWENDA...
MICHEZO Gwiji wa Soka nchini Ufaransa Marcel Desailly ameiambia Sport1...
Read more
Piastri on pole as McLaren lock out...
SAO PAULO, - McLaren locked out the front row for...
Read more
Trailblazing Transformation: Rebecca Miano Poised to Become...
President William Ruto has nominated former Trade Cabinet Secretary Rebecca...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  MHASIBU WILAYA YA SAME JELA MIAKA 20

Leave a Reply