MASTORI
Bunge la Kenya limepiga marufuku uvaaji wa kaunda suti ndani ya majengo yake huku Spika wa Bunge, Moses Wetangula akisisitiza suti hizo ,pamoja na mavazi ya kitamaduni ya kiafrika hawataruhusiwa tena.
Suti hiyo, ambayo imepewa jina la aliyekuwa Rais wa zamani wa Zambia 🇿🇲, Kenneth Kaunda ,imekuwa maarufu hivi karibuni nchini Kenya 🇰🇪 hasa baada ya Rais William Ruto kuonekana mara kwa mara akiivaa kwenye shughuli rasmi.
Hata hivyo,hatua ya bunge kuzuia matumizi ya suti hiyo imezua mdahalo mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Spika Wetangula, amesema marufuku hiyo inatokana na mitindo mipya ya mavazi inayotishia kanuni ya mavazi ya Bunge ,hatua iliyokasirisha baadhi ya watu wanaojiuliza kwanini mavazi ya kiafrika yanapigwa marufuku na Bunge lenye asili ya Kiafrika.