WATU AMBAO HUTAKIWI KUFANYA NAO TENDO LA NDOA au MAPENZI

0

0:00

MASTORI.

Kufanya tendo la ndoa au ngono siku hizi imekuwa kama usasa pamoja na kwamba kuna miiko yake. Sasa ni bora kuwaepuka watu hawa linapokuja suala hili.

1. Usifanye tendo hili na Mwanamke au mwanaume aliyepo kwenye ndoa.

2. Usijaribu kufanya mapenzi na mwajiri wako hata ikitokea akaamua kukufukuza kazi.

3. MUNGU akikujalia kuwa kiongozi wa watu au ukawa na cheo,usitumie nafasi hiyo vibaya kwaajili ya watu wa chini yako. Hapa ,waathirika huwa ni wasaidizi wa ndani.

4. Usiruhusu kufanya mapenzi na walimu wako mathalani chuoni. Kufanya mapenzi na Viongozi wa chuo ili upate upendeleo wa alama za ufaulu ni kujionyesha huna Maarifa kwenye masomo yako ,kitu ambacho sio kizuri.

5. Usiruhusu kufanya mapenzi na kiongozi wako kwenye kampuni ili akupe motisha ya kuwa wewe ni mchapaji kazi.

6. Kufanya mapenzi na ndugu wa mume au mke ni jambo ambalo limewagharimu wengi. Kama ,unavutiwa nae ni bora umfukuze kwa masilahi ya kesho yako nzuri.

7. Kufanya mapenzi na mwanafunzi mwenzako au jirani ni jambo ambalo litakupa wakati mgumu kwenye maisha yako ya kila siku.

8. Ogopa kufanya mapenzi na mtu wa rafiki yako hata kama wakiachana ,usijaribu kujiingiza kwenye huo moto.

9. MUNGU ameumba tendo la ndoa kuwa kati ya mwanaume na Mwanamke, hata siku moja usijaribu kufanya mapenzi na mtu wa sawa na jinsia yako. MUNGU aliiteketeza Sodoma na Gomora kwa sababu ya jambo hili,jiepushe usiwe miongoni mwa hao.

10. Usiruhusu kufanya mapenzi na ndugu yako au mtoto wako.

11. Usiruhusu kufanya mapenzi na mtu ulie nae kwenye mahusiano, tendo hili lipo kwaajili ya kutengeneza kiumbe au ni nusu ya uumbaji. Tendo la ndoa lipo halali kwa wanandoa pekee.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  MAMBO 4 YANAYOHARIBU MAHUSIANO

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading