HABARI KUU.
Rais wa mpito nchini Chad 🇹🇩, Mahamat idriss Deby Itno amemteua aliyekuwa kiongozi wa upinzani, Success Masra kuwa Waziri Mkuu atakayehudumu katika kipindi cha utawala wa kiraia katika taifa hilo ambalo limekuwa katika utawala wa kijeshi tangu Aprili 2021.
Masra ambaye alirejea nchini humo kutoka uhamishoni mnamo Novemba 2023 baada ya makubaliano ya maridhiano alikuwa akipinga utawala wa kijeshi uliotwaa madaraka baada ya kifo cha Rais Idris Deby Itno ,aliyeongoza taifa hilo kwa takribani miaka 30.
Success Masra
Hata hivyo, inaelezwa kuwa vyama vingine vya upinzani vimeonesha kutokubaliana na hatua ya uteuzi huo na kudai kuwa uteuzi wa Masra kujiunga na Serikali ya mpito atakuwa amekubaliana na uvunjwaji haki ikiwemo mauaji ya raia walioandamana kupinga utawala wa kijeshi.