0:00

MAPENZI

Kusema la ukweli, huwa kuna muda wanandoa wanachokana jambo ambalo ni la kawaida kulishuhudia.

Sasa ikitokea au kabla ya kutokea chochote haya ni mambo ya kuzingatia:-

1. Usiwe mtu wa kuongea kumaliza.

Kumtusi mwenza wako matusi ya nguoni yaweza kutengeneza hasira zisizoisha.

2. Kuwa mtu wa kuomba msamaha.

Dharau zinatia kinyongo moyo lakini kujishusha na kuomba msamaha kunatia faraja kwa wawili wapendanao.

3. Usijifanye umezeeka.

Kuwa mtu ambaye unatoka na kuwa karibu na familia yako ,cheza na watoto wenu usikae na kujiona kwamba huwezi kucheza na watoto wenu.

4. Ishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Maisha haya huwa yanakupa hofu na pia ni maisha yaliyojaa huruma na upendo.

5. Usiwe karibu na watu wenye mawazo hasi juu ya ndoa.

Watu ambao hawana ndoa ni watu hatari zaidi.

6. Muwe na mazungumzo nje ya majukumu.

Ni vema kukumbushana majukumu ya kifamilia lakini sio muda wote,mnatakiwa kuongea hata mambo mengine kama siasa na mpira. Muda mwingi ukitumika kwa ajili ya kukumbushana majukumu huwa unaleta kero kwenye mazungumzo.

7. Jiepushe kutenda makosa ya mara kwa mara

8. Fanya mapenzi mara nyingi Kadri unavyoweza.

Tendo ili linapaswa kufanyika kama chanzo cha furaha pia.

9. Kusafiri sehemu mbalimbali.

Safarini mtaona mambo mapya na mtajifunza kuishi vizuri pia.

10. Ucheshi na utani kwa mwenza wako liwe ni jambo la kawaida.

11. Uwe ni mtu wa toba mbele za MUNGU.

Toba itakuweka karibu na MUNGU, maombi yako yatajibiwa kwasababu ya mawasiliano mazuri na MUNGU wako.

12. Usiwe muoga hasa kwa mambo ambayo yako nje ya uwezo wako. Kujiuliza utaishije? Itakuaje?

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  5 THINGS SEX DOESN'T DO

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading