HABARI KUU.
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye amesema atawasaidia vijana wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika kupambana na adui yao.
Katika mkutano na vijana amefahamisha kuwa adui wa Burundi na CONGO ni Rwanda kwahiyo wanapaswa kupambana na adui ili waweze kumshinda.
Pia ameinyoshea kidole Rwanda kwa kuwa chanzo cha usalama mdogo unaoripotiwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
“Tulifunga mipaka kwasababu walitudanganya na wanaendelea kuwahifadhi waasi wa nchi wa Red Tabara “
Amesema Evariste Ndayishimiye.
Matamshi hayo hayajawafurahisha viongozi wa Rwanda ambapo kupitia mtandao wa kijamii wa X Balozi wa Rwanda nchini Uholanzi, Olivier Nduhungirehe amesema kuwa matamshi yake yanaashiria Mapinduzi dhidi ya Rwanda.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.