JINSI YA KUKAA KWENYE MAHUSIANO AU NDOA KWA MUDA MREFU

0:00

MAPENZI

Kila mtu anapenda kuwa kwenye mahusiano au ndoa kwa muda mrefu lakini hali za kimaisha ndio huwa ni mwamuzi wa watu kutengana.

Sasa ni kipi kifanyike?

1. KUAMINIANA.

Usiwe mtu ambaye hutabiriki kwa mwenza wako. Ratiba zako na muda wako ni vitu ambavyo,mwenza wako anatakiwa avijue. Kumfanya mwenza wako mtumwa wako kwa kufatilia mambo yako bila kujua ukweli ni kutengeneza ombwe kwenye mahusiano yenu.

2. MAWASILIANO YA SIMU.

Mpe muda mwingi mpenzi wako wa mawasiliano ya simu hasa unapokuwa mbali nae. Tuma ujumbe labda kwenye WhatsApp au mpigie WhatsApp, umuone. Hii huwa inaleta ukaribu wenu.

3. ELEZEA HISIA ZAKO.

Wakati mwingine, Mpenzi wako huenda akawa haoni umuhimu wa penzi lenu sasa ni muda sahihi wa kumweleza ukweli nae avae viatu vyako kwa jinsi unavyojisikia anavyokuwa anakuchukulia kawaida. Hii, inaweza kumrudisha kihisia hata kama alitaka kubadili mawazo yake kwako.

4. KUWENI NA MAONO SAWA.

Fungua ukurasa wa kumweleza mpenzi wako juu ya maisha yenu ya baadaye, sababu za nyinyi kuwa pamoja, kwanini mko pamoja na mnalenga nini? Haya ni mambo ambayo huleta mvuto kwasababu kila mmoja atajua wajibu wake.

5. PANGA RATIBA YENU.

Mnapokuwa pamoja kwenye mahusiano ni vizuri kuweka muda sahihi kwenye mambo yenu, mathalani mmepanga kuvalishana Pete ya uchumba ni vizuri kuweka tarehe au siku au mwezi au mwaka husika ili wakati huo ukifika basi jambo lifanyike. Mnapoweka muda maalumu na kutimiza jambo lenu basi ,upendo huwa unaongezeka.

6. SALI KWA PAMOJA.

Kumpenda mtu aliyepo mbali ni ngumu. Mnapokuwa karibu, ebu jiweke kwenye mikono ya MUNGU. Pale mlipo wawili na MUNGU yuko katikati yenu. Mtegemee MUNGU kwa mambo yenu.

7. MKUMBUSHE MPENZI WAKO MLIPOTOKA.

Jambo ili ni mtego kwa aliyeko kwenye mahusiano au ndoa. Ebu ,fikiria unamkumbusha mke au mumeo kipindi mnalala chini kabla ya kununua vitanda na vitu vingine vya thamani! Kumbukumbu hiyo inaweza kumrudisha kihisia kwako ,akakumbuka jinsi mlivyovumiliana kwenye shida na raha.

8. EPUKA MAJARIBU.

Unapokuwa kwenye mahusiano au kwenye ndoa ni muda sahihi wa kuacha kujiweka kwenye mazingira ambayo yanaweza kuvuruga hisia kwa mwenza wako. Ukiwa ni mwanaume, jiweke kando na wanawake wengine baki tu na mtu wako.

9. JIBORESHE WEWE BINAFSI.

Pamoja na kwamba huko kwenye mahusiano au ndoa kuna mambo ambayo unatakiwa kuyaweka vizuri wewe mwenyewe. Ikitokea ukapata mwenza ambaye anakushauri vizuri basi zingatia ushauri wake na ufanyie kazi. Unaweza ukashauriwa kwenye suala la usafi basi ndio muda sahihi wa kuhakikisha unajiweka sawa ili usiwe kero kwa mwenza wako.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  AINA 12 ZA WANAUME NA TABIA ZAO.

Related Posts 📫

SABAYA AMBWAGA DPP KORTINI
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
OFFSET AĢAWA INTERNET NA MAVAZI ATLANTA ...
NYOTA WETU. Offset ameweka heshima nyumbani kwao Atlanta alipotembelea huko siku...
Read more
8 SPIRITS THAT CAUSE DELAY IN MARRIAGE...
BOY-FRIEND The last thing on a Boy's Mind is Marriage.Boys don't...
Read more
DON'T TELL ANYONE ABOUT YOUR PARTNER
In A Relationship, Whether Married or still in Courtship, there...
Read more
I actually feel sad for Davido now...
The reason is because, his music career will gradually fade...
Read more

Leave a Reply