MAPENZI
1. Acha kujiuliza mambo mengi yasiyo na maana.
2. Omba msamaha. Kuomba msamaha sio ujinga ni kujishusha na kutaka maisha yaendelee kama awali.
3. Achana na mambo ya kujizeesha. Ndoa inamilikiwa na wenye nguvu, haijalishi una umri gani lakini ukiwa kwenye ndoa unatakiwa kuwa mpya au Kijana au binti. Wamama wakizaa watoto basi wengi hapa huwa wanajisahau.
4. Kwenye ndoa tanguliza uwepo wa MUNGU kwanza. MUNGU ndiye mwenye ndoa ,ikabidhi ndoa yako mikononi mwa MUNGU daima.
5. Jitahidi upate muda mwingi na mwenza wako hata kama una shughuli nyingi. Ndoa itenge na shughuli zako .
6. Unapokuwa ndani ya ndoa sio muda sahihi wa kujenga urafiki na watu wenye maono na maoni hasi juu ya ndoa.
7. Furahia maisha ya ndoa yako na mwenza wako. Cheka,tazama michezo ya TV na mpenzi wako hasa michezo ya kuwapa furaha.
8. Wekeza kwenye mazungumzo ya kawaida sio kila mara unapenda kuzungumza kazi au majukumu yako,kwani kufanya hivyo upunguza furaha au kuleta kero.
9. Epuka mambo ambayo husababisha makosa. Kama simu ndio husababisha mgombane basi ni vizuri kuiweka mbali unapokuwa na mwenza wako.
10. Fanya tendo la ndoa mara nyingi Kadri mnavyoweza . Tendo la ndoa linaleta ukaribu hasa kwa wapendanao.
11. Mitoko ya hapa na pale na mwenza wako ni muhimu ili kurudisha mapenzi yenu.
12. Fanya toba. Kumuomba Mwenyezi MUNGU msamaha wa dhambi ni kufungua masikio ya MUNGU asikilize maombi na Sala zako. Maombi baada ya toba yanamfikia MUNGU moja kwa moja, kwahiyo ni muda sahihi wa kuiombea ndoa yako.
13. Usiogope hasa kwa yale mambo ambayo huwezi kubadili.
14. Mpongeze mwenza wako anapofanya jambo zuri. Pongezi urudisha tabasamu na furaha kwenye ndoa.