HABARI KUU
Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya Dunia kwenye mbio za marathon, Kelvin Kiptum raia wa Kenya Amefariki Dunia kwenye ajali iliotokea jana Februari 11,2024.
Kiptum (24) alifariki pamoja na kocha wake Gervais Hakizimana raia wa Rwanda, katika ajali hiyo mbaya iliyotokea eneo la Kaptagat karibu na barabara ya Elgeyo Marakwet-Revine.
Kamanda wa polisi wa eneo hilo la Elgeyo Marakwet, Peter Mulinge amesema ndani ya gari hilo kulikuwa na watu watatu ambao ni Kiptum, kocha wake na msichana mmoja aliyejulikana kama Sharon Kogsey,ambaye amenusurika kwenye ajali hiyo. Kamanda huyo alisema Kiptum alikuwa akiendesha gari hiyo aina ya Toyota Premio wakati wakielekea eneo la Eldoret.
Mwanariadha huyo aliweka historia hiyo mwaka 2023 kwenye marathon za kilobits 42 Chicago nchini Marekani akimaliza kwa saa mbili na sekunde 35. Huku akitajwa kama mpinzani wa karibu wa mwanariadha mkongwe Eliud Kipchoge.
Wanariadha hao walikuwa ni miongoni mwa wanariadha wa Kenya ambao wangeshiriki kwenye mashindano ya Olympic ya Paris Ufaransa.