HABARI KUU
Nchi ya Rwanda imeituhumu Marekani kwa kuikosoa na kupotosha ukweli kuhusu machafuko yanayoendelea Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Katika tangazo ambalo limetolewa na Rwanda kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, nchi hiyo inaishutumu DRC kwa kuwa chanzo cha mgogoro unaoendelea baada ya Serikali ya Rais Tshisekedi kuongeza idadi ya askari jeshi Kaskazini mwa nchi hiyo.
Wizara hiyo imefahamisha kuwa imekuwa ikijaribu njia ya Kidiplomasia kuzungumza na DRC kutatua mgogoro uliopo lakini juhudi zao ziligonga mwamba.
Rwanda inasema kauli ya Marekani inapotosha ukweli, na kuongeza kuwa hatua za kutuma wanajeshi DR Congo zinatishia usalama wake na ina haki ya kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya tishio hilo.