WANANCHI WAKERWA NA SAFARI ZA TINUBU NA RUTO

0:00

HABARI KUU

Wakosoaji nchini Kenya na Nigeria wameeleza wasiwasi wao juu ya idadi ya safari za nje zinazofanywa na ma-Rais wa nchi hizo William Ruto na Bola Tinubu.

Gazeti la The Standard la nchini Kenya limembatiza Rais Ruto jina la “Rais anayeruka” huku likisema kuwa pamoja na hali ngumu nchini, Rais huyo ameendelea kuzipa kipaumbele safari za nje.

Kwa upande wa Nigeria Kiongozi wa Upinzani Bw.Atiku Abubakar amesema kuwa nchi hiyo haihitaji Kiongozi ambaye ni “Mtalii Mkuu” anayesafiri sana nje huku nchi ikizama kwenye magumu.

Naye mchambuzi wa sera za mambo ya nje nchini Kenya Profesa Macharia Munene ameeleza kuwa baadhi ya safari zina umuhimu lakini zingine hazina umuhimu ni za kujitukuza.

Kampuni binafsi inayosimamia matumizi ya Serikali nchini Kenya imeeleza kuwa bajeti ya safari za ndani na nje imekuwa juu ukilinganisha na uongozi uliopita, na imeongezeka kwa asilimia 30 kulinganisha na matumizi ya mwaka jana.

Aidha ma-Rais hao pamoja na wasemaji wao wameeleza kuwa safari hizo si ubadhirifu bali ni moja ya hatua za kujaribu kuyatatua matatizo yaliyopo nchini.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

BAYERN MUNICH SIGNS MAX EBERL AS SPORTING...
SPORTS Bayern Munich on Monday announced the signing of Max...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA HIVI LEO
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Duale Defends Military Deployment During June 2024...
In his vetting as the nominee for Environment Cabinet Secretary,...
Read more
SABABU YA KIFO CHA GADNER HABASH MTANGAZAJI...
NYOTA WETU
See also  VYUO 20 BORA NCHINI TANZANIA
Mtangazaji maarufu wa kituo cha radio cha...
Read more
KLABU YA BRIGHTON YAWEKA REKODI YA FAIDA...
MICHEZO Klabu ya Brighton imetengeneza faida iliyoweka rekodi ya Pauni...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply