WACHEZAJI NYOTA WALIOWAHI KUKATAA KUSAJILIWA NA REAL MADRID

0

0:00

MICHEZO

Sio rahisi kwa mchezaji mkubwa kukataa nafasi ya kucheza kwenye timu yenye mafanikio makubwa zaidi barani Ulaya kama Real Madrid. Lakini wapo watakaokataa kwasababu hakuna kinachopendwa na kila mtu.

Hawa hapa wachezaji 5ļøāƒ£ Bora waliowahi kupiga chini ofa za Real Madrid šŸ‡ŖšŸ‡ø

1ļøāƒ£ LUIS SUAREZ šŸ‡ŗšŸ‡¾
“Wawakilishi wangu waliongea na Real Madrid na kila kitu kilikuwa kinakaribia kukamilika, nilipopokea ofa ya Barca, nikaenda kwasababu ilikuwa ni timu ya ndoto zangu”

2ļøāƒ£ DAVID VILLA šŸ‡ŖšŸ‡ø
Mwaka 2008 akiwa Valencia, David Villa alipiga chini ofa ya kujiunga na Real Madrid, miaka miwili baadae akajiunga na Barcelona.

3ļøāƒ£ NEYMAR šŸ‡§šŸ‡·
Akiwa na umri wa miaka 13, Neymar alitembelea Bernabeu na kufanyiwa vipimo vya afya ili ajiunge na Real Madrid, wakati huo familia yake haikuwa tayari kuishi mbali na mtoto wao, hivyo wakapiga chini uhamisho huo na miaka kadhaa iliyofuata alikataa ofa yao, akajiunga na Barcelona.

4āƒ£ SANTI CARZOLA šŸ‡ŖšŸ‡ø
ā€œKwenye mpira Kuna mambo mengi sana, ilikuwa ni rahisi kuikataa ofa ya Real Madrid japokuwa ni timu kubwa kwasababu ya kuridhika mahali nilipo na nilikuwa nahisi kuthaminiwa katika klabu yangu ya Villarreal”

“Nilikuwa napenda kuendelea kukua ndani ya Villarreal kwa sababu pia mimi ni mdogo na nimeanza kuitwa timu ya taifa.”

5ļøāƒ£ PAUL POGBA šŸ‡«šŸ‡·
Mwaka 2016, Pogba aliipiga chini ofa ya Real Madrid na kuamua kurejea Manchester United šŸ“󠁧󠁢󠁄󠁮󠁧ó æ akitokea Juventus.

“Moyo wangu ulikuwa unaniambia nirudi Manchester, sijui ni kwa nini, Lakini nilifanya hivyo na sijutii chaguo langu, ingawa, labda inawezekana ulikuwa ni uamuzi mbaya”

UMAFIA WA BWANA PEREZ HAPA ULIKWAMA, HAKUAMBULIA KITU .

See also  Highlights : SIMBA 3-1 TANZANIA PRISONS" on YouTube
Neymar Jr
Paul Pogba
Santi Carzola
David Villa
Luiz Suarez
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading