DANI ALVES AHUKUMIWA KIFUNGO JELA

0:00

MICHEZO

NYOTA wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil, Dani Alves amehukumiwa kifungo cha miaka minne na miezi 6 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumnyanyasa kingono mwanamke mmoja katika klabu ya usiku ya Barcelona mnamo mwaka 2022.

Uamuzi huo umefanywa na Mahakama kuu Nchini Uhispania ambayo sambamba adhabu hiyo imemuamuru beki huyo wa zamani wa Barcelona alipe euro 150,000 kwa mwathirika.

Alves (40) alikuwa ameshikilia kuwa ngono hiyo ilikuwa ya makubaliano. Mwendesha mashtaka alikuwa akitaka kifungo cha miaka tisa jela.

Hii ni mojawapo ya kesi zenye hadhi ya juu zaidi nchini Uhispania tangu sheria iliyopitishwa mwaka wa 2022 kufanya idhini kuwa kipengele muhimu katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia na kuongeza muda wa chini wa jela kwa mashambulizi yanayohusisha unyanyasaji.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SHAKIB TAKES NEW BABY TO BED WHILE...
ENTERTAINMENT ...
Read more
French Court Grounds Naija's Air Force One,...
In a plot twist that sounds more like a Nollywood...
Read more
President Bola Tinubu on Thursday in Abuja...
The President spoke at the Presidential Villa when he received...
Read more
MZEE RUKHSA AMEONDOKA BILA DENI
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Mshukiwa wa Mauaji ya Wanawake 42 Akamatwa
Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanaume mmoja anayefahamika kama Jomaisi Khalisia...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  EMMANUEL AMUNIKE ATEULIWA KOCHA MKUU NIGERIA

Leave a Reply