BITEKO AZUIA LIKIZO ZA WAFANYAKAZI WA TANESCO

0:00

HABARI KUU

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko, amesitisha likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) hadi hapo hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme itakapoimarika.

Dkt. Biteko amechukua hatua hiyo akiwa wilayani Kilombero, mara baada ya kutembelea mtambo wa kuzalisha umeme unaotumia maji wa Kidatu.

Amesisitiza kwamba kwa sasa watumishi wote wajikite kutafuta njia mbadala za kuimarisha nishati hiyo kwa wananchi.

Aidha amesema serikali inakusudia kuunda timu maalumu itakayoshirikisha Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na vyombo vyote vya ulinzi na usalama ili kuongeza nguvu katika usimamizi wa rasilimali maji ambayo yanategemewa kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji wa umeme nchini.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema maelekezo hayo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati yatatekelezwa mara moja na kuwataka maofisa mabonde kuacha kukaa ofisini, badala yake watumie muda mwingi kufuatilia mienendo ya maji katika mabonde yao.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SIRI YAFICHUKA FAMILIA YA LOWASSA KUMBANIA KIKWETE...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Howe hails players' focus as Newcastle revive...
Newcastle United manager Eddie Howe praised his team's hard work...
Read more
President Tinubu Gives Finance Minister 48 Hours...
President Bola Tinubu has instructed the Minister of Finance, Wale...
Read more
BOMOA BOMOA KUANZA APRILI 12 DAR ES...
HABARI KUU Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano Kati ya Benki...
Read more
RAIS SAMIA SULUHU ZIARANI KOREA KUSINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  JE NI NINI KINASABABISHA MFULULIZO WA MAPINDUZI YA KIJESHI KWENYE SERIKALI ZA AFRIKA?

Leave a Reply