UFAHAMU MSIKITI MKUBWA ZAIDI BARANI AFRIKA

0:00

HABARI KUU

Rais wa Algeria Abdelmajid Tebbourne siku ya Jumapili alizindua Msikiti Mkuu wa Algiers, ambao ni msikiti mkubwa zaidi barani Afrika.

Msikiti huu ni wa tatu kwa ukubwa duniani, nyuma ya misikiti miwili iliyopo Maka na Madina.

Msikiti huo umejengwa katika eneo lenye ukubwa wa hekari 70 na unaweza kuchukua waumini 120,000.

Msikiti huu pia una mnara mrefu zaidi duniani.

Unatarajiwa kutumiwa wakati wa mwezi wa Ramadhan unaoanza wiki mbili zijazo.

Msikiti huu ulijengwa kwa muda wa miaka saba na kugharimu zaidi ya dola milioni 800.

Ujenzi wa msikiti huu ulikuwa mradi wa Rais wa zamani wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ambaye aliondoka madarakani baada ya nia yake ya kutaka kuwania urais kwa muhula wa tano kusababisha maandamano makubwa.


Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

TUNDU LISSU AMSHTUKIA MBOWE KUELEKEA 2025
HABARI KUU Baada ya Lissu kutangaza jukwaani kuwa rushwa imekithiri...
Read more
Lazarus Kambole na sakata la Young Africans...
MICHEZO Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Lazarus Kambole ameiweka pabaya Klabu...
Read more
MAGAZETI YA LEO 2 AGOSTI 2023
Dar es salaam Hujambo ? Karibu kwenye kurasa za mbele...
Read more
TONALI AFUNGIWA MIEZI 10 KISA KUBET ...
MICHEZO Kiungo wa Newcastle United, Sandro Tonali amefungiwa miezi 10...
Read more
MWANARIADHA KIPTUM AFARIKI DUNIA ...
HABARI KUU Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya Dunia kwenye mbio za...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  POLISI YATANGAZA MSAKO WA MADADA POA VYUONI

Leave a Reply