MADAKTARI WAZAWA WATENGANISHA WATOTO MAPACHA WALIOUNGANA

0

0:00

HABARI KUU



Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa mara nyingine imeandika historia kwa kufanya upasuaji mkubwa wa kuwatengenisha watoto mapacha waliokuwa wameungana sehemu ya tumbo na kifua na kuwa upasuaji wa kwanza kufanywa na madaktari wazawa hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Rachel Mhaville amesema upasuaji huo umefanikiwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kununua vifaa tiba vya kisasa pamoja na kuwasomesha wataalamu.

ā€œTunachojivunia katika upasuaji huu ni kuwa umefanywa na timu ya madaktari wazawa, umefanyika kwa mafaniko makubwa na watoto wanaendelea vizuri kabisa. Lakini pamoja na kufanikiwa kufanya upasuaji huu bado tutaendelea kushirikiana na wataalamu wengine kwa ajili ya kuendelea kupata ujuzi zaidi na kuendeleza uhusianoā€ amesisitiza Dkt. Mhavile.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Victor Ngota ameeleza kuwa upasuaji wa kuwatenganisha watoto unahitaji utaalamu wa hali ya juu hivyo ulihusisha jopo la wataalamu mbalimbali ikiwemo madaktari bingwa ikiwemo wa upasuaji watoto, upasuaji rekebishi, wataalamu wa usingizi ,wataalamu wa lishe pamoja na wataalamu wa radiolojia.

ā€œ Tuliwapokea watoto hawa tarehe 11 Machi 2023 hivyo tulianza mchakato wa kuwahusisha wataalamu ambao wanahusika na huduma hizi, ilituchukua takribani muda wa miezi kumi kuangalia mwenendo wao wa afya kwa ujumla kabla ya kuwatenganisha ili kuweza kupata dira ya namna watakavyoishi mara baada ya kutenganishwaā€ amefafanua Dkt. Ngota.

Upasuaji huo umefanyika kwa muda wa takribani saa sita hadi kukamilika ambapo ni wa kwanza kufanywa na mdaktari wazawa hapa nchini na kuwa upasuaji wa nne kufanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

See also  Rais wa Liberia Joseph Boakai ametangaza kuwa atapunguza mshahara wake kwa 40%.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading