SHULE KUMI GHALI ZAIDI TANZANIA

0:00

MAKALA

SHULE KUMI GHALI ZAIDI TANZANIA.

International School of Tanganyika (IST)
— Hii ndio shule ghali zaidi nchini. Iko jijini Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. IST hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 34 kwa chekechea hadi shilingi milioni 71 kwa sekondari, kwa mwaka.

2. Braeburn International School
—Hii ni shule ya kimataifa ambayo iko Dar Es Salaam na Arusha. Hufuata mfumo wa IB na ada yake kwa mwaka ni kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 20 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 43 kwa sekondari.

3. Dar Es Salaam International Academy (DIA)
—Hii ni shule ya tatu kwa kuwa na ada ghali zaidi nchini. Iko Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. Ada yake kwa mwaka ni kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 40 kwa sekondari.

4. Iringa International School (ISS)
— Iko mkoani Iringa na hufuata mitaala miwili ya IB na ule wa Cambridge. Hutoza ada kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 17 kwa Chekechea hadi milioni 27 kwa sekondari.

5. Saint Constantine International School
—Inapatikana mkoani Arusha na hufuata Mtaala wa Cambridge. Ada yake ni kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 8 kwa Chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa sekondari.

6. Kennedys House Schools
—Shule za Kennedys ziko maeneo mengi duniani. Nchini Tanzania iko katika mkoa wa Arusha wakiendesha Chekechea na Shule ya Msingi. Ada zao huanzia Shilingi za Kitanzania milioni milioni 8 kwa Chekechea hadi milioni 22 kwa Shule ya Msingi. Shule hii hufuata Mtaala wa Cambridge.

7. Haven of Peace Academy (HOPAC)
—HOPAC ipo katika Jiji la Dar Es Salaam. Hufuata Mtaala wa Cambridge na hutoza ada kati ya shilingi za Kitanzania milioni 16 hadi 22 kwa mwaka.

8. Aga Khan Primary & Secondary School
—Shule hii iko katika Jiji la Dar Es Salaam, na hufuata Mtaala wa IB kama ilivyo ISM. Hutoza ada kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 7 hadi milioni 20.

9. Internation School Moshi (ISM)/ UWC East Africa
— Hii ndio shule ghali zaidi katika mkoa wa Kilimanjaro. Hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 16 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 41 kwa wale wa kidato cha tano na sita. Shule hii hufuata Mtaala wa Internation.

See also  MADHARA YA KUVUTA SHISHA KWA BINADAMU
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

CAFCL ROBO FAINALI:YANGA VS MAMELODI,SIMBA VS AL...
MICHEZO Klabu ya Yanga SC itakutana na Klabu ya Mamelodi...
Read more
Obrey Chirwa afunguka mazito na mipango ya...
MICHEZO “Kitendo changu cha kushangilia kilikuwa ni kuzifikishia ujumbe timu...
Read more
MIKEL ARTETA BADO ANA IMANI YA KUTWAA...
MICHEZO Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta amesema inawezekana timu...
Read more
Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini England Jack Grealish...
Grealish amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara katika...
Read more
GUARDIOLA KUMRITHI SOUTHGATE ENGLAND
Michezo Chama cha soka England (FA) kinatazamia kumpa kandarasi Mkufunzi wa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply